Wezi 2 watoboa shimo kwenye ukuta wa duka na kuiba mali ya thamani la laki 7

Walikuwa wamekodisha chumba kwenye loji inayopakana na duka hilo na usiku ndio walianza kutoboa shimo kwenye ukuta wa duka.

Muhtasari

• Wezi hao wawili walikuwa wamekodisha chumba kwenye loji inayopakana na duka hilo na usiku ndio walianza kutoboa shimo kwenye ukuta wa duka wakiwa ndani ya chumba cha gesti.

• Tukio hilo liinaswa kwenye CCTV  lakini bado hakuna mtu hata mmoja ameshikwa kufuatia wizi huo.

Shimo kwenye ukuta
Shimo kwenye ukuta
Image: Maktaba

Wezi wawili walinaswa katika mkanda wa CCTV wakichimba shimo katika ukuta wa duka moja ya kuuza vifaa vya kielektroniki kabla ya kuiba mali yenye thamani inayotajwa kuwa zaidi ya laki saba.

Tukio hilo liliripotiwa katika eneo la Kitengela, viungaji mwa jiji la Nairobi ambapo video hiyo ilionesha wanaume wawili ambao wamevalia nadhifu wakichimba shimo kwenye ukuta kabla ya kufanay wizi huo wa ajabu.

Kulingana na jarida moja la humu nchini, wawili hao walikodisha chumba katika loji moja iliyoko kando na duka hilo la kuuza simu na vifaa vingine vya kielekroniki mwendo was aa kumi alasiri ya January 12.

Wanaarifiwa kuwa huenda walichukua takribani saa 8 kuchimba shimo hilo kwenye ukuta kabla ya kufanikisha dili lao la wizi.

“Picha za CCTV zilizoonekana na Nation zinaonyesha wanaume wawili waliovalia nadhifu wakiingia katika eneo la duka kuu kutoka upande wa nyuma saa 5.08 asubuhi. Walipora duka na kuondoka saa 6.20 asubuhi na bidhaa. Mshukiwa wa kwanza anaonekana akijipenyeza kwenye tundu, alizima moja ya kamera za CCTV kisha akamuashiria mwenzake kuingia pia,” Nation waliripoti.

Mmiliki wa vyumba hivyo vya wageni ambapo wawili hao walichukua mapumziko kabla ya kupanga uvamizi wao alisema kuwa mmoja wao alikuwa ni mteja wake wa mara kwa mara ambaye alikuwa kila muda anapenda kupewa chumba namba 106.

Baadae ilifahamika kuwa maelezo ya utambulisho wao ambayo waliacha katika loji hiyo wakati wanaomba chumba yalikuwa ya kughushi.