Wakenya wanaogopa jeshi la Uganda-Muhoozi adai

Aliandika kwenye Twitter siku ya Ijumaa akidai kuwa jeshi la Uganda linaweza kuteka Nairobi ndani ya wiki moja.

Muhtasari
  • Hii si mara ya kwanza kwa mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni kuandika ujumbe kuhusu kuiteka Nairobi
KWA HISANI
KWA HISANI
Image: Muhoozi Kainerugaba

Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni Jenerali Muhoozi Kainerugaba amedai kuwa Wakenya kadhaa wanaogopa jeshi la Uganda.

Muhoozi alisema Wakenya wanajua kuwa jeshi la Uganda ni kubwa kuliko la Kenya.

Aliandika kwenye Twitter siku ya Ijumaa akidai kuwa jeshi la Uganda linaweza kuteka Nairobi ndani ya wiki moja.

"Baadhi ya Wakenya wanatuogopa kwa sababu wanajua jeshi letu ni kubwa kuliko lao. Jeshi letu linaweza kukamata Nairobi baada ya wiki 1!" alisema.

Hii si mara ya kwanza kwa mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni kuandika ujumbe kuhusu kuiteka Nairobi.

Oktoba mwaka jana, Jenerali huyo alidai kuwa ingemchukua yeye na jeshi la Uganda chini ya wiki mbili kuuteka mji wa Nairobi.

Katika mfululizo wa jumbe kwenye ukurasa wake wa twitter, Muhoozi alitoa kauli hiyo katika kile ambacho wengi waliamini kuwa ni dhihirisho la nguvu alilonalo yeye na jeshi lake.

"Haingetuchukua sisi, jeshi langu na mimi, wiki mbili kuiteka Nairobi,"Aliandika.