Je, tohara ina athari yoyote katika tendo la kujamiiana?

Kulingana na takwimu takriban mwanaume mmoja kati ya watatu wametahiriwa duniani kote.

Muhtasari

• Idadi kubwa zaidi ya wanaume waliotahiriwa ni Waislamu.

• Katika Uislamu hufanyika kama ibada kwa watoto wachanga wakati wa kuzaliwa Kama ilivyo kwa wayahudi.

Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Wataalam wa upasuaji katika chumba cha upasuaji wakimshughulikia mgonjwa
Image: MAKTABA

Ni upasuaji ambao umefanywa kwa maelfu ya miaka.

Wanahistoria wanaamini kuwa tohara ilikuwepo tangu zamani kama miaka 15,000 katika jamii ya Wamisri na imebaki hadi leo, na takriban mwanaume mmoja kati ya watatu wametahiriwa duniani kote.

Idadi kubwa zaidi ya wanaume hao waliotahiriwa yaani, wale ambao wamekatwa govi la uume,ni kawaida kwa Waislamu, kwa kuwa katika Uislamu hufanyika kama ibada kwa watoto wachanga wakati wa kuzaliwa. Kama ilivyo kwa wayahudi.

Katika nafasi ya pili ni wanaume waliozaliwa Marekani (asilimia 80.5, kulingana na takwimu ya 2016) kwa sababu katika nchi hiyo tohara imekuwa inazingatiwa kuwa na manufaa kwa miongo kadhaa. 

Tohara nyingi duniani hufanywa mara tu baada ya kuzaliwa. Kwa wale ambao hawajatahiriwa inaweza kuwa muhimu baadaye kwa sababu za kiafya.

 

1. Je, kazi ya kibaiolojia ya govi ni nini na nini hutokea wakati inapotolewa?

Govi ni sehemu ya ngozi ya uume inayofunika sehemu ya juu ya uume. Tofauti na ngozi iliyobaki ya uume, ambayo imeshikamana na uume, govi limejitenga na, ikiwa hakuna shida, inapaswa kutolewa hadi uume wote uonekane, katika hali ya ulaini wakati wa uume kusimama.

Sehemu ya ndani wa govi kuwa sawa na sehemu ya ndani ya mdomo au uke wa wanawake.

"Kazi yake ni kufunika kiungo, kutumika kama kifuniko," mtaalamu wa mfumo wa mkojo Ana María Autrán, kutoka Shirikisho la Marekani, anaiambia BBC Mundo.

Wataalam wanaamini pia kuwa inaweza kuwa na kazi fulani ya kinga.

Hata hivyo, Mwanaume anaweza kuishi bila govi.

Lakini sehemu hiyo ya juu ni nyeti sana ya uume.

Wakati govi linapoondolewa kwa sababu za kiafya katika utoto, ujana, au utu uzima, sehemu ya juu ya uume, ambao ulikuwa umelindwa hapo awali, hugusana moja kwa moja na hewa na nguo.

 Kwa sababu hii, katika wiki za kwanza mgonjwa anahisi usumbufu kutokana na nguo. Anaweza, kwa upande wake, kuhisi maumivu wakati wa uume ukisimama.

 Baada ya muda, ngozi ya uume inakuwa ngumu na kupoteza hisia fulani.

 Upasuaji kwa ujumla unafanywa kwa njia mbili: njia ya jadi na upasuaji wa hospitalini ambapo mara nyingi mgonjwa anapewa dawa ya usingizi ili sehemu hiyo nyeti kuweza kukatwa.

2. Ni wakati gani mtu anaweza kufanyiwa tohara?

Ukiacha sababu za kidini na kuzingatia afya, kuna maono tofauti.

Kwa upande mmoja, kuna msimamo wa wengi nchini Marekani kwamba ni vyema kuwatahiri watoto wanapozaliwa. Kulingana na Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto (AAP), "faida za kiafya za tohara kwa watoto wa kiume wanaozaliwa huzidi hatari."

Miongoni mwa faida anazitaja kujikinga na magonjwa ya mfumo wa mkojo, saratani ya uume na kuenea kwa baadhi ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya Ukimwi- VVU.

"Tohara ya wanaume inayofanyika katika kipindi cha mtoto mchanga ina viwango vya chini vya matatizo kuliko inapofanywa wakati wa utu uzima," anaongeza.

Shirika linasema kwamba hakuna ushahidi wa kutosha kuomba ifanyike kwa watoto wote.

 "Ni uamuzi ambao wazazi wanapaswa kufanya, kila mara wakisaidiwa na daktari," daktari wa watoto Ilan Shapiro,mwanachama wa AAP, anaelezea BBC Mundo.

Msimamo wa kinyume unafanyika, kwa mfano, Jumuiya ya madaktari ya Royal Dutch, ambayo inasema kwamba watoto hawapaswi kutahiriwa kwa sababu "hakuna ushahidi wa kutosha kwamba kutahiriwa ni muhimu katika suala la kuzuia magonjwa na kuwa msafi" ,  kwa hiyo "sio." halali isipokuwa kwa sababu za kiafya/matibabu."

"Kinyume na imani maarufu, tohara hubeba hatari ya matatizo ya kiafya na kisaikolojia. Matatizo ya kawaida ni kutokwa na damu, maambukizi na hofu," shirika linasema.

 

3. Je, ina athari yoyote katika tendo la kujamiiana na hisia?

Kwa mujibu wa Shapiro, hili ni swali gumu kujibu, kwani kitakwimu kuna visa vichache vya wanaume ambao wanaweza kulinganisha shughuli zao za ngono kabla na baada ya tohara, hivyo hakuna tafiti zinazothibitisha suala hilo.

Wakati uume ukijirekebisha katika hali yake mpya baada ya tohara, mgonjwa anapata ongezeko la hisia katika uume  ambapo inaweza kusababisha usumbufu, anasema Autrán.

Kisha ngozi ya uume ambayo ililindwa na govi iliyotiwa mafuta- hubadilika inapogusana moja kwa moja na hewa.

"Inaanza kukauka, na wakati ngozi inakuwa ngumu zaidi, unyeti huo hubadilika," Shapiro anaelezea. Anaongeza kuwa govi pia ni eneo lililojaa mishipa ambayo hupotea wakati govi linatolewa.

Baadhi ya wagonjwa huenda hospitalini wakimwomba daktari awatahiri kwa sababu za mapambo: wanaelewa kuwa uume wao utaonekana mzuri zaidi bila kofia ya kinga.

Aina hizi za upasuaji pia hufanyika, kutokana na baadhi ya simulizi: uume hautaonekana mkubwa tena, wala hautakuwa na nguvu zaidi wakati wa ngono. Na hakutakuwa na mbadiliko ya namna ya kumwaga manii. 

Onyo ambalo wataalamu huwapa wagonjwa ni kutoshiriki tendo la ndoa ndani ya wiki nne au tano baada ya upasuaji ili kuepuka maumivu na matatizo ya kuchelewa kupona.

4. Je, inasaidia kuzuia VVU na magonjwa mengine ya zinaa?

 Moja ya faida ambazo wanaokubali tohara wanasema ni kwamba inasaidia kuzuia magonjwa ya zinaa (STDs), kama vile VVU.

 Hata Umoja wa Mataifa, kutokana na mpango wake wa kupambana na VVU, unafanya kampeni kubwa za tohara katika nchi za mashariki na kusini mwa Afrika ambazo zina viwango vya juu vya maambukizi ya virusi hivi.

Uondoaji wa govi umeonyesha kupunguzwa viwango vya maambukizi ya VVU , lakini tu kwa wanaume wa jinsia tofauti na katika maeneo ya maambukizi ya juu.

"Kwamba uhusiano kati ya tohara na maambukizi ya VVU, hauko wazi inaonesha ukweli kwamba Marekani inachanganya kuenea kwa magonjwa ya zinaa na maambukizi ya VVU na asilimia kubwa ya tohara za kawaida. Hali ya Uholanzi ni kinyume kabisa: " ina kiwango cha chini cha maambukizi ya VVU/UKIMWI pamoja na idadi ndogo ya tohara," linasema chama cha matibabu cha nchi hiyo ya Ulaya.

Kwa wanaume wanaojamiiana na wanaume wengine na wanashiriki kikamilifu, ulinzi wa tohara dhidi ya VVU ni sehemu, wakati kati ya wale ambao hawana tofauti hakuna tofauti zilizopatikana.

Magonjwa mengine ya zinaa kama vile kisonono, kaswende, klamidia, malengelenge, virusi vya papiloma ya binadamu au vidonda vya sehemu za siri yamefanyiwa utafiti kwa sababu waliamini kuwa tohara huzuia maambukizi yao. Hata hivyo, hakuna ushahidi wa kuthibitisha hilo.