Jini au mtu?Jamaa asikia harufu ya kidosho aliyekutana naye hata baada ya kuoga

Kulingana na mwanamume huyo alipatana na kidosho huyo siku moja na kisha wakakubaliana kukodisha chumba

Muhtasari
  • Wakati huu au karne hii ya sasa ni tabia ya wanaume na wanawake kuanza uhusiano wa kimapenzi bila hata kujuana vyema

Jamaa mmoja amewaacha wanamitandao wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kusimulia jinsi alivyopatana na kidosho mmoja na kuanza kusikia harufu yake kila wakati.

Kulingana na mwanamume huyo alipatana na kidosho huyo siku moja na kisha wakakubaliana kukodisha chumba cha kulala na kisha wakaanza kujivinjari.

Wakati huu au karne hii ya sasa ni tabia ya wanaume na wanawake kuanza uhusiano wa kimapenzi bila hata kujuana vyema.

Ndio maana visa vingi vya kuvunjwa moyo vimewakumba vijana wengi huku asilimia kubwa wakikata tamaa ya kupenda na kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Huu hapa usimulizi wake;

"Nilipatana na demu nikabisha kisha akakubali  tuaenda guest tukalala,asubuhi tulienda kupima afya tukapata tuko sawa 

Tatiz ni kwamba hata nashindwa kulala vizuri maana harufu yake bado ninayo mwilini,sasa kanipa namba yake ila kasema ni yeye atakuwa akinipigia  sijui ni jini au mtu kanichanganya sielewi 

Nimeoga lakini ile harufu yake ya mwilini hainitoki, nahitaji ushauri,"Alisimuia mwanamume huyo.