Yesu wa Bungoma avunja ukimya kuhusu kusulubishwa siku ya Pasaka

Sherehe za pasaka zitafanyika kuanzia Aprili 7 na kumekuwa na shinikizo kutaka Yesu huyo wa Bungoma kusulubishwa msalabani wakati hyo ukifika.

Muhtasari

• Alisema kuwa tayari Mungu amempa maono ndotoni jinsi atahakikisha hawezi kusulubishwa siku hiyo.

• Mwanamume huyo anayejiita Yesu mwana wa Mungu amekuwa akizua utata huku kipindi kimoja akisema watu 2 tu kutoka Nairobi ndio wataenda mbinguni.

Yesu wa Bungoma azungumzia kusulubishwa pasaka
Yesu wa Bungoma azungumzia kusulubishwa pasaka
Image: Maktaba

Mwanamume kutoka Bungoma anayejiita Yesu wa Tongaren hatimaye amevunja ukimya wake kuhusu uvumi ambao umekuwa ukienezwa mitandaoni kwamba maisha yake yako hatarini kutokana na sehemu ya watu kutana asulubishwe kama Yesu wa Nazareth kwenye Biblia, huku msimu wa Pasaka unapojongea.

Katika video moja ambayo imesambazwa mitandaoni mapema Jumatatu asubuhi, Yesu wa Bungoma ambaye jina lake halisi mwenyewe alikiri kuwa halijui alisema kwamba amesikia madai hayo ila akasema kwamba alilala na kupata ufunuo kutoka kwa Mungu.

Ufunuo upi huo?

Yesu huyo wa Bungoma alisema kwamba Mungu alimjia kwenye ndoto na kumwambia wala hafai kuhofu kwani wale wanaoazimia kumsulubisha njama yao haitafaulu.

Watalala na kwenye ndoto zao wataota na kushangaa ni kwa nini wanamgongelea Yesu misumari, na hapo watagutuka na kutibua njama yao ya kutaka kumsulubishi mtumishi wa Mungu ‘Yesu wa Tongaren’

“Unaona wenye wanaogea mambo ya kusulubisha, sasa leo mzee (Mungu) aliniambia hivi, anaenda kutokezea watu maono wakati wamelala, wakati wanaongea, watakuwa wanaona wanamgongelea Yesu misumari kwa maono, kila mtu anaamka anaanza kushangaa, mbona nagonga Yesu misumari…” Yesu wa Bungoma anaonekana akizungumza kwenye klipu hiyo.

Siku kuu ya pasaka inatarajiwa kuadhimishwa na Wakristo kote duniani kuanzia tarehe 7 mwezi Aprili na mapema wiki jana kulikuwa na taarifa zisizodhibitishwa kwamba Yesu wa Bungoma alikuwa amepiga ripoti polisi baada ya baadhi ya makundi ya watu kujitokeza wakishinikiza kuwa kama yeye ni Yesu wa kweli basi sharti asulubishwe kama ambavyo Yesu mwana wa Mungu kutoka vitabu vitakatifu alivyosulubishwa siku ya Pasaka.

Mwanamume huyo anayejita yesu mwana wa Mungu si mgeni katika masuala ya utata. Kipindi kimoja alinukuliwa akisema kuwa Mungu amempa ufunuo kwamba watu wawili tu kutoka kaunti ya Nairobi ndio watakaokwenda mbinguni.