Alichosema Kioni kuhusu maandamano ya Azimio

Kinara wa Azimio Raila Odinga alitishia kumshtaki Rais Ruto kwa madai kwamba amevunja sheria.

Muhtasari
  • Kulingana naye hawatakubali shinikizo kutoka kwa serikali ya rais William Ruto ili kusitisha maandamano hayo.
JEREMIAH KIONI
Image: ENOS TECHE

Katibu Mkuu wa Jubilee Jeremiah Kioni amejibu kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter kuhusu Maandamano ya Azimio yanayoendelea katika kaunti ya Nairobi na katika baadhi ya kaunti tofauti nchini.

Kulingana naye hawatakubali shinikizo kutoka kwa serikali ya rais William Ruto ili kusitisha maandamano hayo.

"Maandamano ya amani ya kulinda mustakabali wa taifa letu yako kwenye TRACK. Wetu ni msimamo wa UTHUBUTU wa Usawa wa Kiuchumi kwa WAKENYA wote.Hatutaghairi katika vita hii ya UKWELI na HAKI YA KIJAMII."

Mrengo wa Azimio ulifanya maandamano kkwenye kaunti tofauti siku ya Jumatatu.

Huku maandamano yakiwa yameshika kasi baadhi ya wanasiasa na waandamanji walitiwa mbaroni.

Kinara wa Azimio Raila Odinga alitishia kumshtaki Rais Ruto kwa madai kwamba amevunja sheria.

Raila aliandamana na Kalonzo Musyoka,Ledama Ole Kina,Martha Karua,Makau Mutua,Babu Owino,Gladys Wanga,Peter Salasya miongoni mwa viongozi wengine.