Mke aelekea mahakamani akitaka talaka kwa sababu mbegu za mume wake ni majimaji

Wawili hao walikuwa wameoana kwa miezi miwili na kulingana na mwanamke huyo, kila mara walipokuwa wanashiriki tendo la ndoa alikuwa anagundua kwamba manii ya mumewe ni mepesi.

Muhtasari

• Mhojiwa alikubali kuwa alikuwa na maswala ya kiafya, lakini akasisitiza kuwa mke pia alikuwa na changamoto za kiafya.

• Hata hivyo, alisema kuwa bado anampenda mke wake na akaiomba mahakama impe muda wa kusuluhisha sintofahamu hiyo.

Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Mwanaume na mke wasioelewana kwa ndoa
Image: Forbes

Mwanamke mmoja nchini Nigeria ameushangaza ulimwengu baada ya kuelekea mahakamani akitaka ndoa yake kuvunjiliwa mbali kwa kile alisema kuwa mume wake ana mbegu za majimaji.

Kulingana na vyombo vya habari kutoka taifa hilo la Afrika Magharibi linalojivunia idadi kubwa Zaidi ya watu barani Afrika, Salamat Suleiman alikuwa amedumu kweye ndoa na mume wake kwa miezi miwili tu.

Katika kipindi hicho cha miezi miwili, Bi Salamat aligundua kwamba mbegu za mume wake zilikuwa si nzito na mara ya kwanza alifikiria ni jambo lililojitokeza tu kwa mara moja lakini jambo la kushangaza ni kwamab aligundua mbegu hizo zilikuwa majimaji kila mara walipokuwa wanashiriki tendo la ndoa.

Aliomba mahakama ivunje ndoa hiyo, akisema kuwa amechoshwa na uhusiano huo.

Mhojiwa alikubali kuwa alikuwa na maswala ya kiafya, lakini akasisitiza kuwa mke pia alikuwa na changamoto za kiafya.

Hata hivyo, alisema kuwa bado anampenda mke wake na akaiomba mahakama impe muda wa kusuluhisha sintofahamu hiyo.

Jaji mfawidhi, AbdulQadir Umar, alimwambia mke kuwa na mawazo wazi na kutafuta usaidizi wa kimatibabu kwa changamoto zao za kiafya.

Hakimu alimshauri mke huyo kuruhusu nafasi ya pili katika uhusiano huo, akidokeza kwamba ndoa zote zilikuwa na changamoto zake.

Lakini kwa Bi Salamatr, akili zake zilikuwa zimefanya uamuzi na alisisitiza kwamba hakuna kile ambacho angekubali kando na talaka yake tu!

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28 kwa ajili ya kutoa taarifa ya suluhu au kuendelea kusikilizwa.