Mganga wa kienyeji afariki baada ya kunywa dawa alizompa mgonjwa wake na kumuua

Edith mwenye umri wa miaka 59 alielekea kwa mganga Kipoya Chiyesu kupata matibabu baada ya kulalamikia kuvimba mguu, mganga alimpa dawa zikamuua naye akalazimishwa kuzinywa na kufa pia.

Muhtasari

•Baada ya sakata hilo wanakijiji na familia ya marehemu walimfuata mganga awaeleze kilichosababisha ndugu yao kufariki.

• Katika kuthibitisha kuwa dawa aliyompa marehemu haikuwa na sumu wala madhara yeyote na yeye akainywa mbele za watu hao.

Mwili wa marehemu
Mwili wa marehemu
Image: Instagram//Azam

Taifa jirani la Tanzania linafahamika sana kwa kuwa na idadi ya watu wengi ambao wanaamini katika matatizo yao kutatuliwa kwa njia za kishirikina na waganga wa kienyeji.

Siku chache zilizopita, vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamab mwanamke mmoja alifariki dunia baada ya kupewa dawa na mganga mmoja wa kienyeji.

Kwa mujibu wa jarida la Mwananchi, Edith Chilanda mwenye umri wa miaka 59 alielekea kwa mganga kupata matibabu baada ya kulalamikia maumivu ya mguu.

Mganga huyo kwa jina Kipoya Chiyesu alimpa Edith dawa ambazo zilimwendea mrama na kusababisha kifo cha mwanamke huyo ambaye kabla ya kufo chake alianza kutapika na kufariki alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini.

Baada ya sakata hilo wanakijiji na familia ya marehemu walimfuata mganga awaeleze kilichosababisha ndugu yao kufariki.

 

Katika kuthibitisha kuwa dawa aliyompa marehemu haikuwa na sumu wala madhara yeyote na yeye akainywa mbele za watu hao, lakini bahati mbaya mganga yakamkuta yaliyomkuta marehemu Chilanda, Mwananchi waliripoti.

 

Kisa hicho cha kusikitisha kilidhibitishwa na mkuu wa mkoa wa Maskazini Magharibi aliyetajwa kwa jina Dennis Moola ambaye alisema kuwa mganga Chiyesu baada ya kunywa dawa hizo za mitishamba naye alipatwa na dalili kama zile zilizompata Chilanda – kutapika, maumivu ya tumbo kabla ya kuaga dunia pia.

 

"Polisi walitembelea nyumba ya marehemu Chilanda na kukusanya mizizi yote pamoja na mimea iliyokatwa katwa kwenye sufuria ambayo inasadikiwa kuwa waliyotumia marehemu wote," amesema Moola.