Mubaba, 72 amuua kwa risasi mrembo na kujiua pia baada ya kuambiwa mtoto si wake

“Alikuwa na silaha isiyojulikana ambayo aliitoa na kumpiga risasi marehemu upande wa juu wa titi la kulia na kusababisha atoke tundu kubwa.”

Muhtasari

• Kulingana na polisi, Mayonde alikuwa na mtoto wa kiume na Walubita, hata hivyo, wawili hao walianza kutoelewana kuhusu baba wa mtoto huyo.

Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Mwanafunzi ajiua kwa kujipiga risasi Kilimanjaro
Image: YoutubeScreengrab

Mzee wa miaka 72 amemuua mpenzi wake wa miaka 42 na kujitoa uhai baadae baada ya mke huyo kumwambia kuwa mtoto ambaye wamekuwa wakilea pamoja si wa mzee huyo.

Safi Mayonde, 42 anadaiwa kuuawa na Saela Walubita mwenye umri wa miaka 72, aliyedhaniwa kuwa baba wa mtoto huyo mvulana wa miaka 3 ambaye alimfahamisha kuwa si wake.

Kulingana na polisi, Mayonde alikuwa na mtoto wa kiume na Walubita, hata hivyo, wawili hao walianza kutoelewana kuhusu baba wa mtoto huyo.

“Mwanamke huyo alimfahamisha mshukiwa kuwa yeye si baba mzazi wa mtoto. Mnamo tarehe 08/07/23 kati ya saa 10:00 na 13:00, mtuhumiwa alimfuata marehemu shambani kwake ambapo alimkuta akivuna mahindi yake akiwa na watu wengine wawili,” ripoti ya polisi ilisema kama ilivyonukuliwa na jarida la Mwebantu nchini Zambia.

“Alikuwa na silaha isiyojulikana ambayo aliitoa na kumpiga risasi marehemu upande wa juu wa titi la kulia na kusababisha atoke tundu kubwa.”

Mkuu wa polisi alisema polisi walitembelea eneo la tukio na kumpata marehemu akiwa amelala mahali ambapo alipigwa risasi.

“Katika ukaguzi, ilipatikana na tundu kubwa la risasi juu kidogo ya titi la kushoto. Baada ya kupekua eneo la tukio, ganda moja la bunduki lililotumika lilipatikana karibu na mwili huo. Kutoka kwa mashahidi wawili waliokuwepo wakati wa kufyatua risasi, walisema kuwa mshukiwa alimpiga marehemu risasi mara nne,” alisema.

Alisema polisi walianzisha msako wa mtu mshukiwa na alipozuru shamba lake, mshukiwa aliacha ujumbe ulioandikwa kwenye ukuta wa nyumba yake ukiwa na maandishi ya mkaa mweusi akieleza sababu ya kumuua marehemu.

 

"Alikwenda mbali zaidi kuashiria kwamba kwa vile alikuwa amemuua, yeye pia angejiua mwenyewe. Msako ulifanyika kuzunguka shamba lake na mwili wake ambao haukufa ulipatikana ukining'inia kutoka kwa mti umbali wa mita 100 kutoka lango la shamba.”