Raila bado yuko sawa! Wajackoyah asema kuwa Baba asipigwe vijembe kisiasa

Shukrani nyingi kwa Raila Amolo Odinga. Amekuwa na msimamo dhabiti sana,akili yake iko freshi,mawazo yake ni freshi

Muhtasari

• Wajakoyah alisema haya katika mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu Eve Mungai baada ya kutwaa katika uwaja wa ndege wa kimataifa wa JKIA baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea mataifa kadhaa yakiwemo Jamaica kwa mwaliko wa msanii maarufu wa nyimbo za Reggae Richie Spice.

George Luchiri Wajakoyah, Loots Party Picha:HESHIMA
George Luchiri Wajakoyah, Loots Party Picha:HESHIMA

Kinara wa Roots party na aliyekuwa mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2022 George Luchiri Wajakoyah, amesema kinara wa Azimio Raila Odinga bado angali na  uwezo wa kusimama urais wa mwaka 2027.

Wajakoyah alisema haya katika mahojiano ya moja kwa moja na mwanablogu Eve Mungai baada ya kutwaa katika uwaja wa ndege wa kimataifa wa JKIA baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea mataifa kadhaa yakiwemo Jamaica kwa mwaliko wa msanii maarufu wa nyimbo za Reggae Richie Spice.

Haya yanajiri bada ya maswali na mjadala kuibuka kuhusu hatma ya Raila kutaka kiti cha urais mwaka wa 2027 hata baada ya kushindwa kwenye chaguzi mara tano.

Kinara huyo wa Roots party ambaye pia ni mwanachama wa muungano wa Azimio, alisema kwamba kuna haja ya wakenya kubadilisha uongozi ambao umekuwa tangu jadi  akisema kuwa anapendezwa na msimamo wake dhabiti.

"Shukrani nyingi kwa Raila Amolo Odinga. Amekuwa na msimamo dhabiti sana,akili yake iko freshi,mawazo yake ni freshi ila tu kwamba kila anaposimama kwenye uchaguzi, kura zake huibwa."

Ila amewakembea vikali baadhi ya viongozi katika Azimio ambao wana lengo la kumrithi Raila akisema kwamba Raila ndiye kizingi cha chama cha ODM

"Unarithije ODM, Raila ni kama mama wa ODM,na hao wahuni ambao wanakaa karibu na Baba, nataka niwaambie muda wenu umekwisha."

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwapongeza waandishi wa habari kwa kuweka maswala wazi,

"Najivunia sana vyombo vya habari kwa sababu waandishi wa habari ndio watu pekee wanaoleta maana kwa sababu ya jinsi wanavyoweka maswala wazi kwa wananchi."

Alisistiza swala la uongozi akisema kuwa pengine ni wakati kama taifa kuwa na uongozi wa mpito katika bara la Afrika.

"Kipindi cha mpito cha uongozi ndicho tunahitaji kama Afrika,tumechoka kuona watu wale wale kwenye uongozi."

Wajakoyah amewaambia viongozi walio mamlakani waepuke swala la kushirikiana na polisi kuwanyanyasa watu ka kuwakata kiholela bila sababu akisema kwamba wanapaswa kujua kuwa wanwakatisha tamaa watu wanaowaongoza.