Mrembo aripotiwa kupoteza ujauzito saa 3 tu baada ya kuonesha mimba yake TikTok

"Nilipoteza ujauzito saa 3 baada ya kuipakia kwenye TikTok. Watu waovu kila mahali. Weka tu usiri wako, nimepoteza mtoto wangu,” aliandika.

Muhtasari

• Mwanamke huyo aliyevunjika moyo alinukuu video hiyo kwa ujumbe wa kugusa moyo, akisisitiza hitaji la faragha licha ya mikasa isiyotazamiwa.

Mrembo apoteza mimba.
Mrembo apoteza mimba.
Image: TikTok

Mtumiaji wa TikTok kutoka Nigeria anayeitwa @urfavoriteesangirl amefunguka kwa machozi kuhusu kupoteza mimba yake.

Msichana huyo ambaye alitarajia kuwa mama hivi karibuni alifichua katika video hiyo yenye hisia kwamba furaha yake iligeuka na kuwa huzuni saa tatu tu baada ya kuchapisha video iliyoonyesha bonge la mtoto wake kwenye mtandao maarufu wa kijamii.

Video hiyo ya kihisia na ya kugusa moyo ilinasa mwanamke aliyehuzunika hospitalini, ikionyesha huzuni kubwa aliyokuwa nayo juu ya kufiwa kwa ghafla na kuhuzunisha kwa mtoto wake ambaye hajazaliwa.

Katika hali ya kusikitisha, alishiriki habari hizo na wafuasi wake, akiwahimiza kutambua umuhimu wa kuweka mambo ya kibinafsi kuwa ya faragha ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Mwanamke huyo aliyevunjika moyo alinukuu video hiyo kwa ujumbe wa kugusa moyo, akisisitiza hitaji la faragha licha ya mikasa isiyotazamiwa.

Pia alitumia fursa hiyo kuwafungua macho warembo wenzake kuwa amepata funzo japo kwa njia chungu, kwamba si kila mtu katika mitandao ya kijamii inayokutakia mema – wapo wengine wazandiki wanaokuombea shari.

"Nilipoteza ujauzito saa 3 baada ya kuipakia kwenye TikTok. Watu waovu kila mahali. Weka tu usiri wako, nimepoteza mtoto wangu,” aliandika huku akitoa mwanga juu ya udhaifu unaoweza kutokea kutokana na kushiriki matukio ya kibinafsi kwenye mitandao ya kijamii.