Nakuru: Wanandoa wapatikana wakiwa na wanaishi na maiti ya dada yao kwa wiki 3

“Hiyo maiti ilikuwa imeanza kuoza, ni kama yawiki tatu hivi, kufunua kitambaa hivi, aaahu, tulipata mama yangu, kichwa kimekuwa fuvu. uncle akaniambia eti 'usijali atafufuka'" mtoto wa marehemu alisema.

Muhtasari

• David Kinyanjui na mkewe wamekuwa na mwili wa dada yao Rosemary Wahu mwenye umri wa miaka 60 kwa wiki tatu huku familia ikimsaka kila kona bila mafanikio.

Picha ya maktaba ya gari la Polisi la Kitengela katika eneo la uhalifu hapo awali.
Image: MAKTABA

Wapelelezi wa DCI kaunti ya Nakuru wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa cha kushangaza ambapo wanandoa walipatikana wakiwa wanaishia na maiti ya dada yao ambaye anakisiwa kufariki wiki tatu zilizopita.

Wanandoa hao ambao wapo mikononi mwa polisi wanaarifiwa kuishi na maiti hiyo huku Nakuru Mashariki na maiti ya mpendwa wao bila kutoa taarifa yoyote.

Kwa mujibu wa ripoti kwenye runinga ya Citizen, Mama Rosemary Wahu alionekana mwisho akiwa hai mwishoni mwa mwezi Januari kabla ya familia yake kufahamu kuhusu kifo chake chenye utata.

David Kinyanjui na mkewe wamekuwa na mwili wa dada yao Rosemary Wahu mwenye umri wa miaka 60 kwa wiki tatu huku familia ikimsaka kila kona bila mafanikio.

“Tulifika 6am tukaka hapa nje tukapiga simu ndio wakafungua. Lakini walikawia kufungua kwa kama dakika 40 hivi ndio wakafungua. Baada ya kuingia, mke wake akatumabia tuombe kwanza kabla ya kwenda kumuona huyo dada yetu,” Gachoka Kanyone, mwanafamilia alisema.

Baada ya kuingia kumuona mpendwa wao, walipigwa na butwaa kuona mwili wa Rosemary Wahu ambao ripoti hiyo ilisema ulikuwa umeanza kuoza na ulikuwa umehifadhiwa kwenye chumba cha kulala.

Boniface Mwania ambaye ni mwanawe marehemu ambaye aliona mwili huo alisema;

“Hiyo maiti ilikuwa imeanza kuoza, ni kama yawiki tatu hivi, sijui ni nani alifunua hicho kitambaa hivi, aaahu, tulipata mama yangu, kichwa kimekuwa fuvu. Tukapiga nduru ndio nikamuuliza binamu wangu, unaweza ua mama yangu, akaniambia usijali, atafufuka.”

Baada ya nduru za rabsha, maafisa wa usalama waliwahi na kuwaokoa David Kinyanjui kutoka mikononi mwa umati uliokuwa umejawa na hasira.

Kamanda wa polisi Nakuru Mashariki Mohammed Wako alithibitisha kukamatwa kwa wawili hao ambao alisema walichukuliwa kwa uchunguzi Zaidi kubaini kiini chao kusalia na maiti ndani kwa muda mrefu bila kupiga ripoti au kuupeleka makafani.