Usikose usingizi ukitaka kufahamu maana ya “Brief Interrogation” – DCI yawaambia Wakenya

Aghalabu, DCI hutumia maneno mazito ya Kiingereza, wakati mwingine semi na nahau zenye maana fiche na ya kuchekesha wakijaribu kuchora taswira ya jinsi tukio lilivyotokea.

Muhtasari

• DCI waliamua kuweka wazi maelezo kamili kuhusu kauli moja ambayo aghalabu wanaitumia baada ya mtuhumiwa kutiwa nguvuni.

DCI
DCI
Image: FACEBOOK//DCI

Wapelelezi wa makosa ya jinai, DCI kupitia ukurasa rasmi wa Facebook wameamua kuwatania Wananchi kuhusu kauli changamano ambazo wanatumia wakati wanatoa maelezo kwa njia ya maandishi kwenye kurasa zao mitandaoni.

DCI waliamua kuweka wazi maelezo kamili kuhusu kauli moja ambayo aghalabu wanaitumia baada ya mtuhumiwa kutiwa nguvuni.

Kila mara wanaporipoti kuhusu mtuhumiwa au mshukiwa kutiwa mbaroni, wanamalizia kwa kauli kwamba amepelekwa mahabusu kwa udadisi wa kina, wakitumia kauli ya lugha ya Kiingereza, Brief Interrogation’.

Sasa DCI wameamua kuielezea kauli hii kwa ufafanuzi na ufaafu Zaidi, na kuwataka Wakenya kutopoteza hamu ya usingizi wakijaribu kuipata maana ya kauli ‘Brief interrogtion’ kwani ni kaui rahisi tu kuielewa.

Walieleza kwamba kwa mujibu wa maelezo ya Google, ‘Interrogation’ ni kumuuliza mtu maswali machache kwa lengo la kutaka kubaini jambo Fulani fiche.

“KWA KUEPUSHA SHAKA. Usipate usingizi usiku juu ya maana ya maneno "Brief Interrogation". Interrogation - kuuliza maswali ya (mtu), wakati mwingine kutafuta majibu au habari ambayo mtu aliyeulizwa anaona kuwa ya kibinafsi au ya siri. (kwa hisani ya Google). Ni hayo tu 🤝🤝🤝.” Walisema.

Tangu waanzishe kurasa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, DCI wamejulikana sana na Wakenya watumizi wa mitandao hiyo kutokana na mbinu ya ucheshi wanayotumia kuripoti kuhusu tukio la kihalifu.

Aghalabu, DCI hutumia maneno mazito ya Kiingereza, wakati mwingine semi na nahau zenye maana fiche na ya kuchekesha wakijaribu kuchora taswira ya jinsi tukio lilivyotokea.