388 wapatikana na corona baadaya sampuli 4,287 kupimwa

Watu 6 wafariki huku 388 wakipatikanana corona

Ongezeko la visa vya maambukizi ya corona vinaanza kuhofisha kwani shule zinafunguliwa jumatatu

Muhtasari
  •  Leo Nakuru inaongoza kwa visa 86 
  • Watu 6 wameaga dunia  na kufikisha idadi  ya walioangamia hadi 766

 

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

 Watu 388 wamepatikana na virusi vya coron baada ya sampuli 4,287 kupimwa katika saa 24 zilizopita na kufikisha visa hivyo hadi sasa kuwa 41,546.Jumla ya sampuli zilizpimwa kufikia sasa ni 591,198.kati ya visa hivyo 383 ni vya wakenya ilhali 5 ni vya raia wa kigeni ,284 ni wanaume ilhali 104 ni wanawake .

 Mgojwa wa umri wa chini ni mtoto wa miaka mine ilhali wa umri wa juu ana miaka 85 .

Nakuru leo pia imeongoza kwa idadi ya visa vingi baada ya kusajili visa 86 ,Nairobi 84,Mombasa 51, Trans-Nzoia 49 ,Kiambu 29, Kisumu 17,Kericho 11,Meru 10,Busia 10, Bungoma 8,Machakos 7,Garissa 5,Kajiado 3,Tharaka Nithi 3,Nyamira 3,Nyeri 2,Siaya 2,Makueni 2,Nandi 2,Kwale 2 na Nyandarua 2

 Watu 63 wamepona ugonjwa huo na kufikisha jumla ya idadi ya waliopona kuwa 31,000.Hata hivyo watu wengine sita wameaga dunia kwa ajili ya corona na kufikisha 766 watu walioangamizwa na virusi hivyo .