Wakili afariki

Wakili ambaye alikatwa mikono na polisi afariki

Nancy Njeri hajashtakiwa

Muhtasari
  •  Wakili huyo alikatwa mikono na afisa wa polisi Nancy Njeri 
  • Uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo

 

Onesmus Masaku

Wakili mmoja aliyekuwa akihudumu huko Makueni ambaye mikono yake ilikatwa na afisa wa kike wa polisi ameaga dunia .

Onesmus Masaku  aliaga dunia siku ya jumapili katika hospitali  kuu ya Kenyatta ambako alikuwa akipokea matibabu  baada ya shambulizi hilo nyumbani kwake Wote  na polisi  constable Nancy Njeri.

 Mwenyekiti wa chama cha LSK  tawi la kusini mashariki Justus Mutisya amesema  Msaku aliaga dunia mwendo wa saa sita  mchana .

Masaku  alikuwa aelazwa katika hospitali ya rufaa ya Wote baada ya shambulizi hilo na baadaye kuhamishwa hadi katika hospitali ya KNH . Alikuwa akiuguza majeraha ya mkono baada ya mikono yake kukatwa . Mutia amemtaka Masaku kama mtu aliyekuwa na bidii na kifo chake kwa ghafla ni  jambo ambalo  limewashtua wenzake .

 Afisa wa Polisi Nancy Njeri wa kituo cha Polisi cha Makueni  hajafikishw akortini  huku polisi wakisema uchunguzi unaendelea .

 Suala hilo litatajwa tarehe 23 oktoba  baada ya polisi kuitisha muda wa siku 14 zaidi kukamilisha uchunguzi wao.