- Rais atakuwa na naibu wake
- Waziri mkuu atakuwa na manaibu wawili
Ripoti ya BBI ambayo imekuwa mada katika ndimi za wengi katika siasa hatimaye imetolewa na mapendekezo yake makuu kudhihirika .
Ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga katika hafla iliyoandaliwa huko Kisii .
Kabla ya ripoti hiyo kutolewa wanasiasa wamedai kwamba ililenga kuvuruga azma ya baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini au kuunda nafasi kuu za uongozi kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022 .
Ripoti hiyo imebadilisha pakubwa muundo wa serikali na bunge b na endapo itapitishwa serikali itapanuliwa ili kuwa na waziri mkuu na manaibu wake wawili .waziri mkuu atakuwa na maamlaka huku mawaziri wakitarajiwa kuteuliwa kutoka kwa wabunge .
Katika ripoti hiyo kundi hilo limependekeza kurejeshwa kwa serikali katika bunge ambapo nafasi za waziri mkuu ,manaibu wawili wa waziri mkuu ,mwanasheria mkuu na kiongozi wa upinzani
Muundo huo ni tofauti na tulicho nacho sasa ambapo rais anasaidiwa na naibu wake .
Upanuzi huo wa serikali unalenga kuhakikisha kwamba jamii zote zinajumuishwa katika serikali ili kuepuka mtindo wa sasa ambapo mshindi huchukua yote .
Chini ya mapendekezo ya kamati hiyo serikali itakuwa na rais ,naibu wa rais ,waziri mkuu ,manaibu wawili wa waziri mkuu na mawaziri .
Mapendekezo hayo sasa yatatosheleza matamanio ya rais Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga kuafikia malengo yao chini ya mwafaka wa Handshake ambao walisaini machi mwaka wa 2018
Raila amekuwa akisisitiza kwamba muundo wa serikali uwe kama mapendekezo yaliyokuwa yametolewa katika katiba ya Bomas .
Katiba ya Bomas ilikuwa imependekeza kuundwa kwa afisi ya rais ambaye ni kiongozi wan chi ,kamanda mkuu wa majeshi na mwenyekiti wa baraza la kitaifa la usalama .
Kulingana na kamati hiyo ,badala ya kuwa na mfumo wa sasa wa urais ,kutakuwa na muundo unaojumuisha afisi ya rais na bunge .