Ndoa za jinsia moja

Papa mtakatifu Francis aunga mkono sheria za ndoa za jinsia moja

Papa Francis atofautiana na msimamo wa awali wa kanisa la katoliki

Muhtasari

 

  •  Amesema mashoga pia ni watoto wa mungu 
  • Amesema misimamo yao haifai kutumiwa kutenga au kuwanyanyasa 

Papa mtakatifu Francis  amekuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa la katoliki kuunga mkono sheria za watu wa jinsia moja

 Papa Francis siku ya jumatano  aliitisha kupitishwa kwa sheria za watu wa jinsia moja  akitofautiana na msimamo wa muda mrefu wa kanisa  hilo  kuhusu suala la ndoa za jinsia moja .

 “ Wapenzi wa jinsia moja wana haki  ya kuwa sehemu ya familia .Ni watoto wa mungu  na hawafai kutupwa nje  au kunyanyaswa kwa ajili ya  mahusiano yao’ amesema Papa Francis

Francis  hapo awali alikuwa ameunga mkono ndoa za  watu wa jinsia moja  alipokuwa  alkofu mkuu wa   Buenos Aires.

 Matamshi hayo yake yanatarajiwa kuzua mjdala miongoni mwa waumini wa kanisa la katoliki .