BBI

Ipoa yaunga mkono mapendekezo ya BBI kuifanya kuwa Mamlaka Huru

ipoa sasa itazisimamia idara nyingine pia za polisi

Muhtasari
  • BBI inataka ipoa kuwa maamlaka huru 
  • Idara za magereza polisi wa utawala na huduma ya polisi zitawekwa chini ya  usimamizi wa IG 

 

Anne Makori mwneyekiti wa IPOA

Mwenyekiti wa Mamlaka ya kusimamia shughuli za polisi IPOA  Anne Makori  amekaribisha mapendekezo yaliyomo katika ripoti ya BBI  ya kuibadilisha IPOA kuwa Mamlaka .

Makori  amesema  iwapo mapendekezo hayo yatapitishwa  itakuwa rahisi kwa majukumu ya IPOA kuzidishwa ili pia kusimamia idara nyingine za usalama na sio Huduma ya polisi pekee .

  Hatua hiyo inamaanisha kwamba kupitia marekebisho ya sheria bungeni  Ipoa itaweza kuzisimamia idara kama vile Magereza  ,KWS  NA Shirika la kulinda Misitu nchini KFS .

 Ili kuhakikisha kwamba polisi wanawajibika katika utendakazi wao  BBI inalenga kuibadilisha  IPOA kuwa mamlaka huru ili kuwachukulia hatua polisi wanaokiuka mikataba ya utendakazi wao 

Makori  amesema mapendekezo hayo ya  BBI yanaipa mwamko mpya IPOA . Pia mapendekezo hayo yanaziweka idara za polisi wa utawala ,magereza na huduma ya polisiu chini ya Inspekta mkuu wa polisi .