- Ruto amesema idara ya mahakama inafaa kuwa huru
- Amesema Polisi hawafai kuingiliwa na wanasiasa
- Alionekana kuendeleza msimamo wake kuipinga ripoti ya BBI
Naibu wa rais William Ruto siku ya jumatatu amejipata pabaya wakato hotuba yake kuhusu mambo yanayofaa kubadilishwa katika ripoti ya BBi ilipowakera baadhi ya wajumbe .
Watu waliokuwa katika ukumbi huo walianza kumtaka Ruto kumheshimu rais . Ruto alikuwa ameratibu baadhi ya mambo yaliofaa kubadilishwa ama kuboreshw akatika ripoti hiyo ya BBI .
Ruto alisema kwamba kuteuliwa kwa afisi ya tume ya mamalamishi ambayo mkuu wake atateuliwa na rais ni kuingilia uhuru wa idara ya mahakama .
Ruto alisema hatua hiyo inaweza kulirejeha taifa katika siku za kale ambapo rais alikuwa akitoa maelekezo kwa majaji kupitia simu . Ruto amesema wakenya wengi wangali wanapata ugumu kuafikia haki na baadhi ya masuala hayo yanafaa kushughulikiwa na katiba . Ruto amesema idara ya mahakama inafaa kupewa ufadhili wa kutosha .
Ruto alikosoa pia pendekezo la kuvitaka baadhi ya vyama vya kisiasa kuwateua makamishna wa uchaguzi . Alijaribu kumpa Raila Odinga mfano kutumia soka akisema mchuano hauwezi kuwa na usawa endapo baadhi ya timu zitaruhusiwa kuwateua marefarii . Raila hata hivyo alionekana kutozingatia ukosoaji huo wa Ruto na kuangalia kando