Mtoto wa BBI?

‘Niko tayari kuwa wako’-Mrembo aliyemchekesha rais Uhuru akisema yuko tayari kupata mtoto wa BBI

Ashura Michael Alisema Raila ndiye atakayechukua mahari

Muhtasari

 

  • 'Najua mama alikubali babangu Raila ako hapa tayari kuchukua mahari'
  • Alikuwa akizungumzia matamshi ya wiki jana ya  rais Kenyatta alipokuwa ziarani Kisumu ambapo  alisema kwamba anazingatia kumtafuta mke wa Pili kutoka eneo hilo

 

Kulikuwa na ucheshi katika ukumbi wa Bomas wakati  mwakilishi wa watu wenye ulemavu wa  kuongea  Ashura Michael alipotoa posa kwa rais Uhuru Kenyatta

"Mheshimiwa Rais recently you went to Kisumu na nikasikia ulikuwa unatafuta mpango wa kando. Najua mama alikubali babangu Raila ako hapa tayari kuchukua mahari na ndugu yangu deputy president akikubali atakuwa bestman," Ashura  alisema kwa utani

 Aliongeza kusema ;

.."Na mama wa taifa tutaendelea kubuild bridges pamoja. Na sasa mtoto wa BBI atazaliwa.

 Usemi wake uliwachangamsha wote katika ukumbi huo walioangua kicheko  huku raus Uhuru akimgeukia Raila  na kupiga makofi naye naibu wa rais William Ruto akionekana pia kufurahishwa na utani wa Mrembo huyo .

 Alikuwa akizungumzia matamshi ya wiki jana ya  rais Kenyatta alipokuwa ziarani Kisumu ambapo  alisema kwamba anazingatia kumtafuta mke wa Pili kutoka eneo hilo

"Nilikuwa naambia Raila hapa jameni... Sijui kama mama nyumbani ataniruhusu... Akiniruhusu labda naweza kupata mtu ambaye atakuwa ananitengenezea mambo yangu pande hii..."  Alisema  katika hotuba yake

"Ndio tuwe tukitembea ukijua kuna mahali utakuwa unakula ugali ama namna gani