- Rais alishangaa mbona Ruto ameanza kampeini za mapema
- Ruto na Rais walionekana wakicheka kuhusu kijembe hicho cha Uhuru
- Uhuru amesema vijana hawafai kuchochewa bali kuhusishwa katika maaamuzi
Rais Uhuru Kenyatta ameonekana kueleza taswira ilivyo kati yake na naibu wake William Ruto kuhusu uchaguzi wa mwaka wa 2022 . Uhuru alionekana kutumia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya BBi kutoa maoni yake kuhusu kinachoonekana na wengi kama hatua ya Ruto kuanza kampeni za mapema za uchaguzi huo .
Uhuru amesema haelewi jinsi naibu wake alisahau kuhusu malengo yao ya Jubilee na kuanza kampeini za uchaguzi huo . Alitoa mfano wa mbio za kupokezana vijiti akisema mwanarioadha anafaa kumpa mwenzake kijiti aendelee kukimbia lakini naibu wake ‘amepinduka na kuanza kukimbia akirudi upande ule mwingine’ matamshi ambayo yalizua kicheko katika ukumbi wa Bomas
"Tulisonga pamoja lakini hapa kati kati ndio sasa 2022 ikaingilIa akasahau yale mengine but nasema tutulize boli..’ Uhuru amesema
"2022 itakuja miaka hairudi nyuma.. Tuko relay, lakini sasa my brother William anapinduka anakimbia nyuma..mos mos.. utafika tu’ Uhuru alisema huku akicheka
Wakati rais alipokuwa akicheka Ruto aliamka kumueleza kitu cha utani na rais akazidi kucheka naye Ruto akirejea katika kiti chake .
Ruto alijipata katika hali isiokuwa nzuri wakati baadhi ya wajumbe katika ukumbi wa Bomas walipoana kumkemea akieleeza mambo ambayo anayapinga kaika ripoti ya BBI .
Uhuru aliendelea na hotuba yake akisema kwamba ‘hatufai kukubali sarakasi ambazo zinaizuia Kenya kufaulu’
" Naamini tunaweza kuafikia mengi na kuipya changamoto hii . tunajifanya sisi ni viongozi wa kitaifa lakini wakati unawpofika tunaanza lugha za mama ….’
Uhuru pia alieleza jinsi suala la vijana linafaa kushughulikiwa vizuri na kwa njia ya ustadi
"... Sio kwa kuwachochea lakini kwa kuwahusisha katika mchakato wa kufanya maamuzi’ alisema rais
" Iwapo tunataka kushughulikia tatizo la vijana kwana tushughulikie uchumi wetu .hakuna uchumi unaostawi kwa kipindi cha miaka mitano ya kisiasa’