Uhuru awashukuru Raila,Ruto

Uhuru : Raila hajawahi kutaka mgao katika serikali

Pia amemshukuru Ruto

Muhtasari
  •  Amesema BBI sio kuhusu kugawana nafasi za uongozi 
  • Amesema Ruto alikuwa sehemu ya mchakato wa BBI na alijua kwamba  anafanya amzungumzo na Raila 
  • Rais amesema lengo ni kuziweka jamii zote serikalini na usawa 

 

Rais Uhuru Kenyatta jumatatu amemshukuru  kiongozi wa ODM Raila odinga kwa kujitolea  kuafikia Amani na mwafaka ili kumaliza uhasama wa kisiasa  kati yao  baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2017

 Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti ya BBI katika ukumbi wa Bomas , Rais alisema haikuwa rahisi kwao kuanza mazungumzo kwa sababu ya ushindani mkali uliokuwepo wakati wa uchaguzi

‘ Tulipoanza kuzungumza , tulikubaliana kwamba hatukuwa hapo kugawana nafasi na tukaweka  vyeo vyertu kando’

 ‘Ajenda yetu ya pamoja ilikuwa kumaliza ghasia za uchaguzi kama ilivyoshuhudiwa 1992,1997,2007 na 2017 … tukasema machafuko hayo hayafai kurudiwa tena ‘

 Rais amesema wakati wa mazungumzo yake na Odinga ,Raila hakuwahi kuitisha nafasi serikali au kutaka mgao ndani ya serikali

Amesema ‘ Hata tunavyozungumza leo ,hayuko serikalini ,hajawahi kutoa  ombi la kutaka kuwa serikalini…. Alisema tushirikiane ili tushughulikie madhila ambayo huleta uhasama aili siku zijazo tushindane bila umwagikaji wa damu ya wakenya … nataka kukushukuru Raila  kwa moyo wangu wote kwa ulichofanya  kwa sababu haikuwa ni lazima ufanye hivyo..’ Uhuru  amesema

 Uhuru pia amemshukuru naibu wake William Ruto akisema kwamba wakati wa mchakato huo mzima wa kuzungumza na Odinga ,rais alikuwa akimfahamisha Ruto kuhusu kilichokuwa kikiendelea

‘ …Alikuwa(Ruto) sehemu ya yote yaliyokuwa yakifanyika ..ni ukweli…sisemu wongo …yuko hapa muulizeni .. Hata alinisaidia kutawatambua baadhi ya wazee hawa niliowateua katika kamati ya BBI’ Uhuru amesema

 Rais Uhuru ameserma alimweleza Ruto kwamba mazungumzo yake na Raila yalikuwa  na kuzidishwa kwa hatua ya mwafaka ambayo yeye na Ruto walikuwa wamefanya mwaka wa 2013 wala haikuwa kuhusu kitakachofanyika katika chaguzi za siku zijazo .

‘Nilitaka tuwe na mazingira ambapo hakuna mkenya anaachwa nje ama nyuma ya utawala au serikalini … na nilijiambia nitatumia siku ya leo kama siku ya kuwashukuru …’