- Mwalimu huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mombasa kwa siku 11 zilziopita na alizikwa mwendo wa saa tisa alasiri
- Shule zote mbili za Star of the Sea na Tononoka secondary zimefungwa . Masomo hata hivyo yameendelea katika shule ya upili ya Mama Ngona licha ya visa kuripotiwa
Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tononoka Moahammed Khamis ameaga dunia kwa ajili ya Covid 19 /Kifo chake kinairi siku moja tu baada ya shule hiyo kufungwa kwa ajili ya ripoti za kusambaa kwa ugonjwa huo katika shule ya Tononoka .
Naibu wake Benjamin Kitsao Nzaro amethibitisha kicho cha mkuu wake akisema marehemu alikuwa amelazwa hospitalini mjini Mombasa wiki jana .Ameaga dunia jumatatu alasiri .
Mwalimu huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mombasa kwa siku 11 zilziopita na alizikwa mwendo wa saa tisa alasiri .
Masomo katika shule mbili za upili huko mombasa yalikatizwa wiki jana baada ya walimu 15 kuambukizwa virusi hivyo .
Kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo alisema walimu 11 kutoka shule ya upili ya Tononoka na wanne kutoka Mama Ngina High School walipatikana na vrusi vya corona .
Kitiyo amesema sampuli zimechukuliwa kutoka kwa waloimu wa shule ya upili ya Star of the Sea baada ya kuripotiwa kwa visa vya ugonjwa huo katika shule hiyo .
Shule zote mbili za Star of the Sea na Tononoka secondary zimefungwa . Masomo hata hivyo yameendelea katika shule ya upili ya Mama Ngona licha ya visa kuripotiwa
Afisa mkuu wa afya wa kaunti ya Mombasa Pauline Oginga amesema usimamizi wa shule ya Star of the sea ilikuwa imetaka kuchukuliwa kwa sampuli ili zifanyiwe vipimo .
Waziri wa elimu George Magoha ameonya dhidi ya kufunguliwa kwa shule baada ya watu 931 kupatikana na virusi hivyo siku ya jumapili . Akizungumza mjini Nairobi Magoha amesema baraza la mawaziri halijaidhinisha uamuzi wa shule zote kufunguliwa .