- Murkomen amesema rais anafaa kuzungumza na viongozi wote
- Amedai kwamba kuna njama ya kuitumia BBI kuwagawanya wakenya
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amemshtumu rais Uhuru Kenyatta kwa kuigawanya nchi kupitia mchakato wa siasa za BBI
Kupitia twitter seneta huyo amesema Uhuru anafaa kutumia maafikiano katika kuhakikisha kwamba mapendekezo ya BBI yanapitishwa bila kuzua mgawnayiko miongoni mwa wakenya .
" Nataka kumrai rais Uhuru akome kuligawanya taifa . rais anafaa kuwa kiongozi wa wote na kujifunza kuwanganisha wakenya na sio hii dhana ya ‘utafanya nini’ Murkomen amesema
Alikuwa akijibu posti moja ya Ikulu kutangaza mkutano kati ya rais Uhuru Kenyatta a wabunge wanaounga mkono BBI mjini Naivasha .
Viongozi kutoka bunge na senate wamekuwa wakikutana Naivasha ili kujadili masuala tata katika ripoti ya BBI .
Washirika wa Uhuru na kiongozi wa ODM Raila Odinga wamekuwa wakiitisha kupitishwa kwa ripoti hiyo bila marekebisho ilhali washirika wa naibu w arais William Ruto wanataka baadhi ya mapendekezo hayo kujadiliwa na kufanyiwa marekebisho .
Kauli yake iliungwa mkono na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung'wa, aliyesema kwamba mchakato wa BBI unatumiwa kuwagawanya wakenya ili kuafikia ajenda ya kisiasa