- Rais Uhuru amesema Wamarekani wametoa sauti yao kupitia kura
- Biden amesema ni wakati wa kuiponya Marekani baada ya mgawanyiko wa kisiasa
- Donald Trump amezidi kushikilia kwamba hajashindwa katika uchaguzi huo
Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa kumhongera rais mteule wa Marekani Joe Biden kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa Marekani .
Uhuru ametaja ushindi wa Biden kama ishara ya wamerakani kuwa na matumaini na uongozi wa makamu huyo wa zamani wa rais .
" Wamerakani wamezungumza kwa sauti kupitia kura zao kwa kumchagua kiongozi mwenye uzoefu mkubwa kuwa rais wao’ amesema rais Kenyatta
" kwa niaba ya watu na serikali ya Kenya namhongera Biden na makamu wake Kamala Harris kwa ushindi wao wanapojitayarisha kungoza Amerika…’
Rais amesema Biden ni rafiki wa Kenya ambaye ziara yake ya mwisho nchini ilikuwa akiwa makamu wa rais wa Barack Obama ilisaidia kuimarisha uhusiano kati ya Kenya na Marekani
Rais alimhongera Harris kwa kuandikisha historia baada ya kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia nafai hiyo ya pili ya uongozi nchini Marekani .
Kwa upande wake kiongozi wa ODM Raila Odinga pia alimhongera Biden kwa ushindi wake akisema Kenya inangoja kushirikiana naye atakapoanza kuiongoza Marekani
" Tunatarajia kushirikiana kuhusu changamoto kubwa za ulimwenguni ikiwemo kukabiliana na corona,kudorora kwa uchumi na mabadiliko ya hali ya hewa.Kila la heri’ amesema Odinga .
Biden amesema ni wakati wa ‘kuiponya’ Amerika katika hotuba yake ya kwanza baada kutangazwa kuwa mshindi siku ya jumamosi huku rais Donald Trump akikataa kukubali matoeo na kupa kupinga matokeo yalimweka Bden kileleni kupitia kesi mahakamani .