Ufisadi

Asilimia 63 za kesi za ufisadi zapelekea kuhukumiwa kwa washukiwa katika nusu ya mwaka wa 2020

Haji asema wamefauku katika vita dhidi ya rushwa

Muhtasari

 

  •  Idadi ya kesi  zilizotamatika kwa watuhumiwa kupatwa na hatia zilikuwa  7, 27, 35, 43  na  45  mwaka wa 2015, 2016, 2017, 2018  na 2019  mtawalia
  •  Vita dhidi ya ufisadi  ni mojawapo ya mambo muhimu ambayo ofisi hiyo imeangazia kati ya januri mwaka wa 2018 na Juni mwaka huu .
  • Jumla ya kesi 26  zilisajiliwa  kufikia juni tarehe 26  mwaka huu  huku kesi 78 zikiripotiwa mwaka wa 2019  na kesi 116 zikiripotiwa mwaka wa 2018

 

DPP Norrdin Haji

Kesi 220 za ufisadi ziliwasilishwa kortini kati ya januari mwaka wa 2018 na Juni mwaka huu ,kulingana na mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Haji .

 Kulingana na  ripoti iliyotolewa na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma  idadi ya kesi ambazo ofisi hiyo imeshinda imeongezeka pakubwa  kati ya mwaka wa 2017 na 2020.

 Vita dhidi ya ufisadi  ni mojawapo ya mambo muhimu ambayo ofisi hiyo imeangazia kati ya januri mwaka wa 2018 na Juni mwaka huu .

 DPP amesema kwamba idadi ya watuhumiwa wanaopatikana na makosa mahakamani ni mojawapo ya vigezo vinavyotumiwa   kukadiria  mafanikio ya kupambana na ufisadi .

" Tumeshuhudia ongezeko la  idadi ya kesi ambazo watuhumiwa wamepatikana na hatia kwa asilimia 63.16 katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2020’

 Idadi ya kesi  zilizotamatika kwa watuhumiwa kupatwa na hatia zilikuwa  7, 27, 35, 43  na  45  mwaka wa 2015, 2016, 2017, 2018  na 2019  mtawalia

 Kiwango cha kupatikana na hatia kilikuwa  30.4%, 46.55%, 37.63%,47.25%  na  47.27%  katika miaka ya  2015, 2016, 2017, 2018 na  2019  mtawalia " Haji  amesema

 Jumla ya kesi 26  zilisajiliwa  kufikia juni tarehe 26  mwaka huu  huku kesi 78 zikiripotiwa mwaka wa 2019  na kesi 116 zikiripotiwa mwaka wa 2018

 Jumla ya kesi 238 zilikimilishwa  huku 20 zikikamilishwa kufikia juni tarehe 30 mwaka  huu ,kesi 103  mwaka wa 2029 na kesi 115 mwaka wa 2018