Mwanakandanda Mohamed Salah apatikana na virusi vya corona

Muhtasari
  • Mchezaji Mohamed Sala apatikana na virusi vya covid-19
  • Hii ni baada ya kuhudhuria harusi na kuonekana bila maski wakati huo
mo salaha golden shoe
mo salaha golden shoe

Klabu cha mpira cha Liverpool kimepokea pig kubwa baada ya mmoja wa wachezaji wake Mohamed Sal kupatikana na virusi vya covid-19.

Kupitia kwenye ukurasa wa twitter wa Sky Sports News ilithibitisha kuwa mchezaji huyo amepatikana na maambukizi ya corona.

"Mohamed Salah amepatikana na corona, FA ya misri imthibitisha."

 

Salah alikuwa miongoni mwa wachezaji watakao chuana na timu ya Togo Jumamosi,14 Novemba katika kitengo cha Egypt AFCON, lakini kwa sasa hatakuwepo kwa maana  amepatikana na virusi hivyo.

Pia ilisemekana kuwa mwanakandanda huyo hakuwa na dalilizozote za virusi hivyo.

Kwa wakati mwingine Sala alihudhuria harusi ambao alionekana kama hajavalia maski, mwanakandanda huyo amekuwa na bidii huku msimu huu akifungia timu ya Liverpool magoli kumi.

Liverpool imejinyakulia nafasi ya tatu katka jedwali ya ligi kuu.