Trafiki

Polisi wa trafiki kukubali leseni za kidijitali za kuendesha magari

Hata hivyo una saa 24 kuwasilisha leseni yenye stakabadhi

Muhtasari

 

  •   Hata hivyo baada ya kuonyesha leseni ya kidijitali ,mwenye gari ana saa 24 kutoa leseni halisi katika kipindi cha saa 24 .
  • Msimamo huo wa IG  ni tofauti na walichosema polisi mwaka jana . Polisi mwaka wa 2019 walisema kwamba wanaokosa kuonyesha leseni ya kuendesha gari inapoitishwa na polisi wa trafiki watatozwa faini zisizozidi shilingi elfu kumi

 

Mutyambai
IG Hillary Mutyambai Mutyambai

Wenye magari wapo katika hatari ya kupigwa faini ya shilingi 1000 wanaposhindwa kuthibitisha kwamba wana leseni za kuendesha gari .

Wakati wa maswali na majibu kwa inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai siku ya jumatatu , Mkuu huyo wa polisi amesema  wenye magari sasa wanaweza kuonyesha leseni za kidijitali ili kuthibitisha kwamba wamepewa leseni kuendesha magari .

  Hata hivyo baada ya kuonyesha leseni ya kidijitali ,mwenye gari ana saa 24 kutoa leseni halisi katika kipindi cha saa 24 .

 “ Iwapo huna leseni yenye stakabadhi  unaweza kumuonyesha polisi leseni  yako ya kidijitali  ..ukikosa kufanya hivyo unajitia katika hatari ya kupigwa faii ya shilingi 1000’ amesema Mutyambai

 Alitoa maelezo hayo baadaya mtu mmoja kutaka kujua kinachofanyika anaposahau kuibeba leseni yake .

 Hata hivyo msimamo huo wa IG  ni tofauti na walichosema polisi mwaka jana . Polisi mwaka wa 2019 walisema kwamba wanaokosa kuonyesha leseni ya kuendesha gari inapoitishwa na polisi wa trafiki watatozwa faini zisizozidi shilingi elfu kumi

 Kulingana na kipengee cha 105 cha sheria za trafiki ,polisi anaruhisiwa kuingia katika gari lako  na kuliendesha iwapo atashuku kwamba uhalifu ama kosa limetendeka .

Mutyambai vile vile amewatahadharisha wakenya dhidi ya kuabiri matatu ambazo hazifuati kanuni ziliwekwa na wizara ya afya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona .