BBI

Uzinduzi wa ukusanyaji wa saini za BBI wafutilia mbali

Tarehe mpya itatangazwa baadaye

Muhtasari

 

  • Hafla hiyo ilitarajiwa kuandaliwa siku  ya alhamsi .
  •  Taarifa hiyo imetiwa saini na wenyeviti wa pamoja  Denis Waweru na mbunge wa Suna mmashariki  Junet Mohamed .

 

Kiongozi wa ODM Raila Odinga

 

  Hafla ya uzinduzi wa sahihi za kutumiwa kufanikisha mswada wa BBI ili kutoa nafasi ya kuandaliwa kwa kura ya maoni imeahirishwa . Hafla hiyo ilitarajiwa kuandaliwa siku  ya alhamsi .

 Kupitia taarifa siku ya jumatano  kamati ya kitaifa ya kusimamia mchakato wa BBI imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kuchelewa kuchapishwa kwa  mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 .

 Taarifa hiyo imetiwa saini na wenyeviti wa pamoja  Denis Waweru na mbunge wa Suna mmashariki  Junet Mohamed .

 Wawili hao wamesema kwamba kamati ya usimamizi inashughulikia tarehe mpya ya kuzindua ukusanyaji wa saini hizo milioni moja .

 Hatua hiyo imejiri baada ya rais Uhuru Kenyatta kuandaa mkutano na naibu wake William Ruto  kwa saa tatu  katika ikulu ya Nairobi . Gazeti la The Star linaripoti kwamba wawili hao walijadili ripoti ya BBI na jinsi ya kushughulikia matakwa ya naibu wa rais William Ruto ambaye amezua pingamizi kuhusu baadhi ya mapendekezo katika ripoti hiyo .

 Rais Kenyatta amekuwa akisema panafaa kuwa  na mwafaka  kuhusu mapendekezo ya ripoti hiyo lakini mshirika wake  wa Handshake Raila Odinga amekuwa akisema kwamba hapana fursa ya kuirekebisha ripoti hiyo .

 Odinga alikuwa ametangaza hafla ya  alhamisi akisema yeye na rais Uhuru wangeongoza uzinduzi wa ukusanyaji wa saini na alitaka zoezi hilo kukamilishwa kufikia jumanne wiki ijayo .

 Kundi la BBI linalenga kukusanya sahihi milioni moja kutoka kwa wakenya kwa matayarisho ya kura ya maoni .

 Sahihi hizo kisha zitawasilishwa kwa tume ya uchaguzi ili kuthibitishwa na kisha mswada maalum kuwasilishwa kwa mabunge ya kaunti  ndani ya kipindi cha miezi mitatu