Odinga hakushtuliwa na marekebisho ya BBI

ODM yakana kwamba Raila aliachwa gizani kuhusu marekebisho katika mswada wa BBI

Muhtasari
  • Kuna ripoti kwamba Odinga hakufahamu kuhusu baadhi ya marekebisho katika ripoti ya BBI 
  • Mswada wa BBI hata hivyo umeondoa pendekezo kwamba vyama vya kisiasa ndivyo vitakavyowateua makamishna wa IEBC

 

 Chama cha ODM  kimekanusha ripoti kwamba kiongozi wake Raila Odinga aligutushwa na marekebisho katika mswada wa BBI .

Msemaji Dennis Onyango  siku ya alhamisi amesema Raila alihusika na marekebisho hayo  ili yaambatane na mswada wa marekebisho ya katiba mwaka wa 2020.

 “ Raila  alitumia hafla ya hapo jana(Jumatano) kuangazia  miswada ambayo ilikuwa imezua utata  pamoja na mapendekezo ambayo yaliachwa nje ‘ Onyango amesema

  Wakati wa uzinduzi wa shughuli ya ukusanyaji sahihi Raila alisema ;

" Wengi ambao mumekuwepo mnafahamu kwamba uchaguzi unaowza kutajwa kama uliokuwa sawa a wa wazi ulikuwa wa mwaka wa 2002 .Makamishna walioteuliwa na rais Moi walikuwa wakiangaziwa na walioteuliwa na vyama vya upinzani’

 Mswada wa BBI hata hivyo umeondoa pendekezo kwamba vyama vya kisiasa ndivyo vitakavyowateua makamishna wa IEBC . Mswada mpya  haujataja hatma ya makamishna wa sasa wakiongozwa na mwenyekiti Wafula Chebukati