Covid-19:Watu 4 wafariki huku 949 wakipatikana na virusi vya corona

Muhtasari
  • Watu 949 wapatikana na virusi vya corona huku 274 wakipona
  • Pia watu 4 wamefariki na kufikisha idadi jumla ya 1,445 ya watu walioaga kutokana na corona
kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kagwe

Watu 949 wamepatikana na virusi vya corona na kufikisha idadi jumla ya 82,605 ya watu waliopatikana na corona.

Hii ni baada ya sampuli 8,311 kupimwa ndani ya saa 24, katika maambukizi hayo mapya 913 ni wakenya huku 36 wakiwa na raia wa kigeni.

Pia 558 ni wanaume na 391 wakiwa ni wanawake, mgonjwa wa umri wa chini ana miezi miwili huku mwenye umri wa juu akiwa na iaka 100 amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe.

 

Huku hayo yakijiri watu274 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 54,399 waliopona corona,224 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 50 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti humu nchini.

Pia watu 4 wamepoteza maisha yao na kufikisha idadi jumla ya 1,445 walioaga kutokana na covid-19.

Wagonjwa 1,244 wamelazwa hspitalini nchini kote huku 7,829 wakiwa wamejitenga nyumbani,78 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi ICU.