DNA

Vipimo vya DNA vyathibitisha kwamba Mbunge Murunga ndiye baba ya mmoja wa watoto wa mpenzi wake

Vipimo vya DNA havikumhusisha mtoto huyo wa kiume .

Muhtasari
  •  Wanapatholojia  M mwangi na Dr.P Maturi wamesema sampuli zilizokusanywa  za DNA zimeonyesha kwamba Murunga alikuwa baba ya mtoto mmoja – wa kike
  • Murunga  aliaga dunia Novemba  tarehe 14  alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya kuanguka na kuzirai akiwa nyumbani kwake

 

Aliyekuwa mbunge wa Matungu marehemu Julius Murunga. (Picha: HISANI)
Aliyekuwa mbunge wa Matungu marehemu Julius Murunga. (Picha: HISANI)

 Sampuli za DNA  zilizopimwa zimethibitisha kwamba marehemu mbunge wa Matungu Justus Murunga ndiye baba ya mmoja wa watoto wa mpenzi wake  Agnes Wangui

Wangui  alikuwa amedai kupitia stakabadhi za mahakama kwamba alikuwa amewapata watoto wawili na marehemu mbunge huyo . mmoja ni mvulana wa miaka saba  na mwingine ni mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 3  .

 Wanapatholojia  M mwangi na Dr.P Maturi wamesema sampuli zilizokusanywa  za DNA zimeonyesha kwamba Murunga alikuwa baba ya mtoto mmoja – wa kike

  Vipimo vya DNA havikumhusisha mtoto huyo wa kiume .

Wangui  na Murunga  walifahamiana kwa miaka saba . walikutana mara ya kwanza mwaka wa 20212 wakati  marehemu alipokuwa akifanya kazi katika shamba la Embakasi ilhali Wangui alikuwa mfanyibiashara  katika eneo la Ruai .

  Wakati huo huo wakili Danstan Omari  jana  amesema atawasilisha kesi kortini  ili kuhakikisha mtoto huyo wa kiume pia ana haki ya kupata Uradhi kwa sababu alikuwa pia akimtegemea Marehemu Murunga .

Murunga  aliaga dunia Novemba  tarehe 14  alipokuwa akipelekwa hospitalini baada ya kuanguka na kuzirai akiwa nyumbani kwake