Kenya Vs Somalia

Kenya haitalipiza kisasi dhidi ya Somalia asema Oguna

wizara hiyo Imesema itashughulikia suala hilo wakati litakapotolewa kupitia taratibu rasmi na zifaazi

Muhtasari
  •  Oguna amesema siku ya jumanne kwamba Kenya haina nia ya kulipiza kisasi kwa kuwaita mabalozi wake kutoka Somalia .
  • Kenya imeonekana kuimarisha uhusiano wake na jimbo la Somaliland ambalo limetangaza kujitawala .
Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna

 Serikali imeunda  kundi  la kutafuta suluhisho kwa mzozo wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia ,amesema msemaji wa serikali Cyrus  Oguna .

 Hii ni baada ya Somalia kutangaza kwamba imekatiza uhusiano  wa kidiplomasia na Kenya kwa kuingilia uhuru wake na masuala yake ya ndani . waziri wa  mashauri ya kigeni wa somalia  Osman Dubbe ametangaza kwamba nchi yake itawaondoa wanadiplomasia wake kutoka Kenya katika siku 7 zijazo ,

 Oguna amesema siku ya jumanne kwamba Kenya haina nia ya kulipiza kisasi kwa kuwaita mabalozi wake kutoka Somalia .

 “ Sisi ni taifa   lenye hadhi ya juu ,hatuwezi kufanya ilichofanya Somalia . tukifanya hivyo itaonekana kana kwamba tunalipiza na hivyo basi tutaziacha IGAD na Comesa zichukue usukani kumaliza mzozo huu’ Oguna amesema

 Wizara ya mashauri ya kigeni imeliambia gazeti la The Star kwamba  Kenya haijapokea mawasiliano yoyote rasmi kutoka kwa Somalia kuhusu hatua yke ya kukatiza uhusiano wa kidiplomasia .

 wizara hiyo Imesema itashughulikia suala hilo wakati litakapotolewa kupitia taratibu rasmi na zifaazi

Kenya imeonekana kuimarisha uhusiano wake na jimbo la Somaliland ambalo limetangaza kujitawala .

 Rais Uhuru Kenyatta hata amefanya mkutano na ujumbe wa nchi hiyo ukiongozwa na rais Muse Bihi  ili kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.rais wa Somaliland pia alikutana na  na mjumbe mkuu wa muungano wa Afrika kuhusu miundo msingi Raila Odinga .