Mutura afanyia mabadiliko baraza la mawaziri la Nairobi

Muhtasari

 • Mutura alilifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.

 •  Janet Ouko aliyejiuzulu baada ya kutofautiana na aliyekuwa gavana Mike Sonko anarejea kama  waziri wa elimu.

Kaimu gavana wa Nairobi Bernard Mutura
Kaimu gavana wa Nairobi Bernard Mutura

Kaimu gavana wa jiji la Nairobi Benson Mutura siku ya Jumatano alifanya mabadiliko ya kwanza katika usimamizi wa kaunti hiyo.

Mutura alilifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri.

Katika madailiko hayo Janet Ouko ambaye alijiuzulu baada ya kutofautiana na aliyekuwa gavana Mike Sonko anarejea katika uliyokuwa wadhifa wake kama waziri wa elimu na maslahi ya vijana.

 

Lucia Mulwa ambaye alikuwa anashikilia wadhifa wa waziri wa elimu amehamishiwa wizara ya kilimo.

Jairus Musumba ameteuliwa kaimu katibu wa kaunti huku Paul Mutungi akiteuliwa afisa mkuu katika afisi ya gavana.

Mutura alisema kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuimarisha huduma kwa wananchi wa kaunti ya Nairobi.

Mutura alichukuwa hatamu za uongozi wa jiji la Nairobi baada ya aliyekuwa gavana Mike Sonko kufurushwa na bunge la kaunti ya Nairobi.

Uchaguzu wa kumteua gavana mpya ulikuwa umeratibiwa kufanyika Februari 18, lakini mahakama iliagiza  kusitishwa kwa mipango ya uchaguzi huo hadi pale kesi iliyowasilishwa na Mike Sonko isikizwe na kuamuliwa.