Ulaghai

Kuhadaiwa: Jamaa aliwapa walaghai shilingi milioni 1 kwa kazi feki ya KDF

Mwanamme huyo aliuza shamba lake na kumpa shilingi 850,000 kisha mshukiwa akatoweka .

Muhtasari
  •  Walifanya mazungumzo mafupi na  Mutitu akamueleza kwamba alikuwa na nafasi katika jeshi aliotaka kumpa mtu  ,hatua iliyotumiwa kumnasa mlalamishi na  kumfanyoa atoe pesa zake .
  •  Mume wake Leonard  alimuarifu Okemer kwamba mke wake ndiye aliyekuwa akisimamia zoezi zima la usajili wa makurutu wa kujiunga na jeshi .
Lucy Catherine Mutitu katika mahakama ya Kibera

Mwanamme mmoja amewailisha kesi kortini baada ya jamaa zake wawili kumfanya uze shamba lake ili aweze kutoa hongo kupata kazi feki ya KDF .

Leonard Etyang Okemer  amesema alidanganywa kuuza shamba lake huko Teso  kwa na kuwapa walaghai shilingi milioni moja . Richard Ouma Okemer na Lucy Catherine  Mutitu  walishtakiwa kaika mahakama ya kibera kwa ulaghai huo .

 Pia walishtakiwa kwa kujifanya kuwa maafisa wa  KDF  kinyume cha sheria na kupokea fedha kutumia wongo .

 

 Uchunguzi wa polisi umeonyesha kwamba Mutitu ameolewa na  binamu ya mlalamishi . Wakati mlalamishi alipokutana naye alijitambulisha kwake kama afisa wa KDF anayehudumu Garissa .

 Walifanya mazungumzo mafupi na  Mutitu akamueleza kwamba alikuwa na nafasi katika jeshi aliotaka kumpa mtu  ,hatua iliyotumiwa kumnasa mlalamishi na  kumfanyoa atoe pesa zake .

 Mume wake Leonard  alimuarifu Okemer kwamba mke wake ndiye aliyekuwa akisimamia zoezi zima la usajili wa makurutu wa kujiunga na jeshi .

Richard Juma Okemer katika mahakama ya Kibera

 Leonard  kisha alielekea Teso na kujifanyakuchukua picha za boma la  mlalamishi huku akimuambia kwamba  tayari alikuwa ameshamuingiza katika jeshi .

 Alisema  sehemu ya fedha hizo zilikuwa za kununua sare za jeshi , dawa ,bunduki  za kufanya mazoezi na risasi . Mwanamme huyo aliuza shamba lake na kumpa shilingi 850,000 kisha mshukiwa akatoweka .

 Uchunguzi ulianzishwa na Mutitu akakamatwa  na kushtakiwa  septemba mwaka jana .Alikana mashtaka dhidi yake mbele ya hakimu mkuu wa kibera Philip Mutua .

 Siku ya jumanne Richard  Okemer alishtakiwa na makosa ya kuchukua pesa kutumia wongo na  kukana mashtaka hayo .

 

 Kesi hiyo itatajwa  jumatano ijayo  ambapo itaunganishwa na ile ya  Mutitu na pia mahakama itaamua kuhusu kuwaachilia washukiwa kwa bondi .