Uchaguzi wa 2022

Raila atakuwa katika ‘debe’ 2022-ODM yathibitisha

Hatua hiyo sasa huenda ikapunguza kipute hicho cha mwaka wa 2022 kuwa makabilianao makali kati ya Raila na Ruto .

Muhtasari
  • Siku ya jumanne Odinga alifanya mkutano na wenyeviti wa matawi yote ya ODM  kutoka kaunti zote katika makao makuu ya chama Chungwa House .
  •  Aliwaambia viongozi hao kwamba ODM itakuwa na mgombeaji wa urais na kutawaka wajitayarishe kwa  kipute kikubwa ambacho alikitaka kama ‘mama ya chaguzi zoite za urais’
Kiongozi wa ODM Raila Odinga

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga  amefufua mkakati kabambe wa kuhaisha azama yake ya kuwa rais  na kuthibitisha kwa mara ya kwanza kwamba atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao .

 Chama hicho kimeanzisha kampeini ya mashinani ili  kumtangaza Raila akama anayefaa kumrithi rais Uhuru Kenyatta atakapokabiliana na naibu wa rais William Ruto  katika kipute hicho kikali .

 Chama hicho kinalenga kufufua matawi yake yote  47 kote nchini ili kuleta uchangamfu miongoni mwa wafuasi wa Odinga na kujaza nafasi za viongozi walikihama ODM na kujiunga na vyama vingine .

 

 Siku ya jumanne Odinga alifanya mkutano na wenyeviti wa matawi yote ya ODM  kutoka kaunti zote katika makao makuu ya chama Chungwa House .

 Aliwaambia viongozi hao kwamba ODM itakuwa na mgombeaji wa urais na kutawaka wajitayarishe kwa  kipute kikubwa ambacho alikitaka kama ‘mama ya chaguzi zoite za urais’

 Katika mahojiano na gazeti la The Star ,maafisa wakuu wa ODM   na walio karibu na Raila  wamethibitisha kwamba Raila atakuwa katika debe  katika ari yake ya kutaka kumrithi rais Uhuru Kenyatta .

 “ Tumeanzisha shughuli zetu .mtu yeyote anayefikiri kwamba  hatupo katika kinyang’anyiro hiki anafaa kujua kwamba tupo’ amesema mwenyekiti wa ODM John Mbadi .

 Hatua hiyo sasa huenda ikapunguza  kipute hicho cha mwaka wa 2022 kuwa makabilianao makali kati ya Raila na Ruto .

 “ Kando na BBI ,Raila  atakuwa akiwania urais 2022.Atakuwa na shughuli nyingi katika siku zijazo’ amesema Mbadi .

 Kampeini za Raila zitategemea ujumbe wa mkataba wake wa kuiunganisha nchi na rais Uhuru Kenyatta kupitia mwafaka wa BBI .