Covid-19:Wagonjwa 28 wako katika ICU huku130 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 130 wapatikana na corona huku 1 akipoteza maisha yake kutokana na corona amesema waziri wa afya Mutahi Kagwe
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Kenya hii leo imesajili visa 130 vipya vya maambukizi ya corona huku maambukizi ya maradhi hayo yakifikia 100,323

Hii ni baada ya sampuli 4,918 kupimwa chini ya saa 24.

Kati ya maambukizi hayo mapya 115 ni wakenya huku 15 wakiwa raia wa kigeni.

 

88 ni wanaume huku 42 wakiwa ni wanawake,mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 4 huku mwenye umri wa chini akiwa na miaka 88.

Vile vile watu 66 wamepona virusi hivyo na kufikisha idadi jumla ya 83,691 ya watu waliopona corona.

Watu 42 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 24 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Wagonjwa 489 wamelazwa hospitalini tofauti humu nchini huku 1,353 wakiwa wamejitenga nyumbani.

Huku hayo yakijiri mtu 1 amepoteza maisha yake kutokana na corona na kufikisha idadi jumla ya 1,751 watu waliada kutokana na corona

Pia wagonjwa 28 wamo katika wadi wa wagonjwa mahututi (ICU).