13 watuma maombi ya kujaza nafasi ya Maraga

Muhtasari

• Tume ya huduma kwa mahakama (JSC) imetoa orodha ya watu waliotuma maombi ya kutaka nafasi ya Jaji mkuu.

• Jumla ya maombi 13 yaliwasilishwa kutaka wadhifa wa jaji mkuu.

• Majaji wanaohudumu katika mahakama ya upeo hawakuwasilisha maombi ya kutaka nafasi ya Jaji mkuu.

Jaji Mkuu David Maraga akishauriana na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Jaji Smokin Wanjala wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 14, 2017. Picha: JACK OWUOR
Jaji Mkuu David Maraga akishauriana na Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Jaji Smokin Wanjala wakati wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, Novemba 14, 2017. Picha: JACK OWUOR

Tume ya huduma kwa mahakama (JSC) imetoa orodha ya watu waliotuma maombi ya kutaka nafasi ya Jaji mkuu na ile ya Jaji wa mahakama ya upeo.

Kulingana  orodha hiyo iliotolewa siku ya Jumatano majaji wanaohudumu katika mahakama ya upeo akiwemo naibu jaji mkuu Philomena Mwilu hawakuwasilisha maombi ya kutaka nafasi ya Jaji mkuu.

JSC mnamo tarehe 20, Januari 2021 ilitangaza kutaka maombi ya wale wanaotaka kuchukuwa nafasi ya Jaji mkuu iliyoachwa wazi na David Maraga aliyestaafu mapema mwaka huu na nafasi nyingine ya jaji wa mahakama ya upeo.

Jumla ya maombi 13 yaliwasilishwa kutaka wadhifa wa jaji mkuu:

  1. Prof Otinga Mare
  2. Prof. Dr. Moni Wekesa
  3. Hon. Mr Justice William Ouko
  4. Hon. Mr. Justice D.K. Marete
  5. Alice Jepkoech Yano
  6.  Hon. Lady Justice Martha Koome
  7. Hon. Mr. Justice Mathew N. Nduma
  8. Ngatia Fredrick SC
  9. Prof Patricia K. Mbote
  10. Philip Kipchirchir Murgor
  11. Said Juma Chitembwe
  12. Otondi Ontweka
  13. Ombongi Brian Matagaro

Watu tisa walituma maombi ya kutaka nafasi ya jaji wa mahakama ya upeo:

  1. Hon. Mr Justice William Ouko
  2. Hon. Mr. Justice D.K. Marete
  3. Alice Jepkoech Yano
  4. Hon. Lady Justice Martha Koome
  5. Hon. Mr. Justice Joseph Sergon
  6. Hon. Mr. Justice Mathew N. Nduma
  7. Hon. Mr. Justice Kathurima M’Inoti
  8. Dr. Justry P. Lumumba Nyaberi
  9. Hon Said Juma Chitembwe

"Tume itaendelea kuorodhesha na kutangaza orodha hiyo ndani ya siku 14 kuambatana na Ratiba ya Kwanza ya Sheria ya Huduma za Mahakama. Tume ya Huduma za Mahakama imejitolea kudumisha utaalam na uadilifu wakati wote wa mchakato wa kuajiri," Katibu wa JSC Anne Amadi alisema.