Covid-19:Watu 105 wapatikana na corona huku 4 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Watu 105 wapatikana na corona huku 4 wakiaga dunia
  • Poa wagonjwa  51 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe

Visa 105 vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumatano baada ya sampuli 3,573 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 104,306 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,269,346.

Kutoka visa hivyo 88 ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 17 . mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 7  ilhali wa umri wa juu ana miaka 82

Wagonjwa 72 ni wanaume huku 33 wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 68 vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Kiambu na visa 12.

Wagonjwa 49 wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 85,626 Watu 34  wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 15 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 4 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla 1,827 ya watu walioga dunia.

Kuna wagonjwa 333 ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,281 wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 51 wapo katika kitengo cha ICU.