Covid-19:280 wapatikana na corona,2 waaga dunia. huku 713 wakipona corona

Muhtasari
  • Watu 280 wapatikana na corona huku 2 wakiaga dunia
  • Huku hayo yakiijiri 713 wamepona maradhi hayo huku 55 wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi
Picha: REUTERS
Picha: REUTERS

Visa 280 vya corona vimeripotiwa nchini siku ya Jumatano baada ya sampuli 4,919 kupimwa katika saa 24 zilizopita .

Idadi hiyo inafikisha 104,780 jumla ya visa hivyo hadi sasa huku sampuli zilizopimwa zikifika 1,278,200.

Kutoka visa hivyo 221 ni wakenya ilhali raia wa kigeni ni 59 . mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 3 ilhali wa umri wa juu ana miaka 89

 

Wagonjwa 173 ni wanaume huku 107 wakiwa wanawake, kulingana na kaunti, kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 185 vipya vya maabukizi ya corona ikifuatwa na kaunti ya Nakuru na visa 19.

Wagonjwa 713 wamepona ugonjwa huo huku idadi hiyo ikifika 86,378 Watu 676 wamepona wakipokea matibabu wakiwa nyumbani huku 37 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Watu 2 wamepoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo na kufikisha idadi jumla 1,839 ya watu walioga dunia.

Kuna wagonjwa 344 ambao wamelazwa hospitalini ilhali 1,495 wapo chini ya mpango wa utunzi nyumbani .

Wagonjwa 55 wapo katika kitengo cha ICU.