Mchekeshaji Eric Omondi atiwa mbaroni kwa kukiuka sheria za tasnia ya filamu

Muhtasari
  • Mchekeshaji Eric Omondi atiwa mbaroni kwa kukiuka sheria za tasnia ya filamu
  • Mchekeshaji huyo atafikishwa kortini kwa kukiuka sheria hizo

Maafisa wa Ufuatiliaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya wakishirikiana na Maafisa wa Polisi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo mchana wamemkamata Eric Omondi  kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Filamu na Maonyesho ya Sura Sura 222 ya Sheria za Kenya kwa kutengeneza na kusambaza filamu zisizoidhinishwa zilizopewa jina la"Wifw material".

Mchekeshaji huyo atafikishwa kortini kwa kukiuka sheria hizo.

Sheria hizo ni kama;

1. Hakuna mtu atakayeonyesha filamu yoyote kwenye maonyesho ambayo umma unakubaliwa au kusambaza filamu hiyo isipokuwa amesajiliwa kama mwonyeshaji au msambazaji na Bodi na kupewa cheti.

2. Hakuna filamu au darasa la filamu ambalo litasambazwa, kuonyeshwa, au kutangazwa, hadharani au kwa faragha, isipokuwa kama Bodi imeichunguza na kutoa hati ya idhini kwa hiyo.

3.Mtu yeyote anayeonyesha filamu yoyote kinyume na masharti ya kifungu kidogo cha (1) au kifungu kidogo cha (2) atakuwa na hatia ya kosa.

Bodi itachukua njia zote zinazowezekana za kisheria kuzuia uzalishaji na maonyesho ya filamu zisizoruhusiwa kwenye jukwaa lolote linalokusudiwa maonyesho ya umma.

Kulindwa kwa watoto kutokana na athariza filamu ambazo ni hatari ni jukumu letu kuu na msanii yeyote anayeunda yaliyomo kwa matumizi ya umma lazima ahakikishe kwamba wanatii masharti ya Sheria ya Filamu katika Sura 222 ya Sheria za Kenya.