Hayati John Pombe Magufuli kuzikwa hii leo Chato Tanzania

Muhtasari

• Maelfu ya wananchi tayari wameanza kujitokeza katika uwanja wa Magufuli ambapo kutakuwa na misa maalumu ya wafu kuombea nafsi ya mwendazake.

• Kabla mazishi mwili wa Magufuli utapelekwa katika kanisani kwa ibada maalumu.

Marehemu rais John Pombe Magufuli
Marehemu rais John Pombe Magufuli

Hayati John Pombe Magufuli ambaye kufikia kifo chake alikuwa rais wa Tanzania anazikwa leo nyumbani kwake eneo la Chato katika makaburi ya familia.

Maelfu ya wananchi tayari wameanza kujitokeza katika uwanja wa Magufuli ambapo kutakuwa na misa maalumu ya wafu kuombea nafsi ya mwendazake.

Kabla mazishi mwili wa Magufuli utapelekwa katika kanisani kwa ibada maalumu.

Rais Magufuli alifariki kutokana na maradhi ya moyo wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam tarehe 17 Machi.

Magufuli ni rais wa kwanza nchini Tanzania kufariki akiwa madarakani na hatua hiyo inalifanya taifa hilo kuongozwa na rais mwanamke kwa mara ya kwanza, Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa siku kadhaa sasa, baadhi ya wakazi wa mji wa Chato na viunga vyake waliokuja kuaga mwili wa rais John Pombe Magufuli. wamelazimika kulala katika mazingira magumu huku wakipigwa na baridi ya usiku kutoka Ziwa Victoria.

Rais Magufuli atakumbukwa kwa kuanzisha miradi kadhaa ya maendeleo nchini Tanzania.

Marehemu kiongozi huyo hata hivyo alijipata katika njia panda na viongozi wengine wa kanda Afrika Mashariki kutokana na vile alikuwa akishughulikia janga la Covid-19.

Chini ya uongozi wake serikali ya Tanzania ilidinda kutoa takwimu za maambukizi.