Dhulma za kingono, jaji Chitembwe ahisi kwamba sheria hiyo inahitaji utathmini upya

Muhtasari

• "Unampelekaje kijana wa miaka 19 kwenda jela miaka 15 kwa kuwa na uhusiano na msichana wa miaka 17?" aliuliza.

Jaji Said Chitembwe akipigwa msasa na makamishna wa tume ya JSC
Jaji Said Chitembwe akipigwa msasa na makamishna wa tume ya JSC
Image: JSC

Jaji Said Kitembwe anahisi kwamba sheria kuhusu dhulma za kingono inafaa kuangaziwa kwa umakini kabla ya uamuzi wowote kutolewa na mahakama ikiwa kuna tuhuma za ubakaji au unajisi.

 Kitembwe ambaye alikuwa akipigwa msasa na tume ya Huduma za mahakama kwa wadhifa wa Jaji Mkuu siku ya Jumatatu alisema kwamba sheria hiyo imekuwa kwa kiasi fulani ikidhalilisha vijana na ndio sababu idadi kubwa ya wafungwa au washukiwa kwenye rumande ni kwa sababu ya madai ya unajisi.

Alielezea msimamo wake kuhusu kesi za unajisi na maswala ya kijamii.

Jaji alisema kuwa licha ya ukweli kwamba sheria inayomkuta yeyote anayemnajisi mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ana hatia lazima izingatiwe uhalali wa suala hilo.

"Unampelekaje kijana wa miaka 19 kwenda jela miaka 15 kwa kuwa na uhusiano na msichana wa miaka 17?" aliuliza.

Jaji Chitembwe katika kesi aliokuwa ameshughulikia hapo awali alikuwa ameamua kuwa msichana alionekana kuwa tayari kufanya mapenzi na mshtakiwa.

Kwa hivyo, alimwachilia huru Martin Charo, 24, ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kufanya mapenzi na mtoto wa miaka 13.

Alisema pia kwamba haendi katika mahakama ya upeo kurekebisha makosa kwa sababu naye hakuna tatizo kubwa. Hata hivyo, alisema ataimarisha mshikamano katika mahakama.

Haya ni mahojiano yake

Kamishna Warsame: Kwa maoni yako hakuna shida kusuluhishwa katika mahakama ya upeo katika utendakazi wake, kisheria.

Jaji Chitembwe: Acha niseme ikiwa kuna shida. Bibilia inasema ikiwa kuna shida nirudishie sawia na Quran.

Kamishna Warsame: Kwa maoni yako hakuna shida kwa misingi ya dhana, uamuzi uliocheleweshwa utatua?

Jaji Chitembwe: Sipendi kuhepa na kwenda kando kila wakati patakuwepo dhana, tafadhali unatatua aje dhana.