Prince Philip: Mwanamfalme Harry atahudhuria vipi mazishi ya Babu yake?

Muhtasari

• Mwanamfalme Harry pamoja na mkewe Meghan Markle walijitoa kushiriki majukumu ya kifalme mwezi Machi Mwaka jana.

• Kwa mujibu wa Kasri la Buckingham, Bi Meghan, ambaye ni mjamzito ameshauriwa na daktari wake asisafiri.

Image: AFP

Mtawala wa Sussex, Mwanamfalme Harry atarejea Uingereza kwa mara ya kwanza wiki hii kuhudhuria mazishi ya Babu yake katika Kanisa la Mtakatifu George ndani ya Kasri la Windsor.

Mwanamfalme Harry pamoja na mkewe Meghan Markle walijitoa kushiriki majukumu ya kifalme mwezi Machi Mwaka jana.

Kama ilivyo kwa wasafiri wengine kutoka nje ya Uingereza, atatakiwa kufuata masharti yote ya serikali kuhusu tahadhari juu ya janga la virusi vya corona.

Mazishi ya Babu yake, ambaye ni mume wa Malkia, Mwanamfalme Philip yatafanyika siku ya Jumamosi.

Je, Meghan atahudhuria mazishi?

Haopana. TMwanamfalme Harry ataungana na Familia ya Kifalme akitokea Marekani ambako anaishi na familia yake bila ya mkewe.

Kwa mujibu wa Kasri la Buckingham, Bi Meghan, ambaye ni mjamzito ameshauriwa na daktari wake asisafiri.

Je, Harry atatakiwa kukaa karantini baada ya kuwasili Uingereza?

Kanuni zilizopo kwa wasafiri wanaoingia Uingereza ni:

  • Kufanya kipimo cha corona siku tatu kabla ya safari na majibu yawe hauna maambukizo.
  • Kujaza fomu ya abiri (kutoa taarifa ya wapi utaishi ukifika Uingereza)
  • Kukaa karantini kwa siku 10 na kufanya vipimo vya Covid-19 siku ya pili na ya nane baada ya kuwasili Uingereza.

Hata hivyo kuna ruhusa ya kuacha baadhi ya kanuni kutokana na hali fulani. Mathalani hautatakiwa kukaa Karantini kama unaingi Uingereza kutoka eneo linalohesabika kaama ni moja katika safari za anga, mathalani nchi ya Ireland.

Karantini ya siku 10 kwa Mwanamfalme Harry haitakuwa katika hoteli (kwa kuwa Marekani haipo katika orodho ya nchi ambazo Uingereza imeziweka katika mstari mwekundu wa hatari ya maambukizo).

Ushauri wa serikali ni kuwa wasafiri kutoka nchi hizo wanaweza kukaa karantini majumbani mwao, "wakiwa na marafiki na famialia" ama katika hoteli au makazi ya muda.

Mtawala wa Sussex pamoja na mkewe wakiwa katika mahojiano na Oprah Winfrey.
Mtawala wa Sussex pamoja na mkewe wakiwa katika mahojiano na Oprah Winfrey.
Image: HANDOUT

Muongozo wa mazishi kwa England - wakati wa marufuku ya kutoka nje - unasema waombolezaji wanaotoka nchi za nje wanaweza kutoka katika sehemu walizojitenga katika mazingira maalumu na kwa sababu za kiubinadamu.

Mazingira hayo ni pamoja na kuhudhuria mazishi ya ndugu wa karibu ama rafiki.

Katika nyakati zote hizo watatakiwa kuhakikisha hawakaribiani na watu wengine na watatakiwa baada ya hapo.

Mwanamfalme Harry pia anaweza kutoka karantini kabla ya siku 10.

Mpango maalumu wa kupima virusi unawaruhusu watu kulipia gharama za vipimo binafsi ndani ya siku tano baada ya kuingia Uingereza - kama majibu yatakuwa hauna maambukizi - basi utaruhusiwa kutoka karantini.

Hata hivyo, ili Mwanamfalme anufaike na mpango huo, itamlazimu kuwasili Uingereza hivi karibuni.