Kenya yasitisha safari za ndege kwenda na kutoka Somalia

Muhtasari

• Katika ilani hiyo, serikali ya Kenya haikutoa sababu zozote za hatua hiyo.

• Marufuku hiyo inajiri siku chache baada ya Qatar kufanikiwa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia katika ya Mogadishu na Nairobi.

Mamlaka ya safari za ndege ya Kenya imesitisha safari zote za ndege kwenda na kutoka Somalia katika arifa ya wahudumu wote siku ya Jumanne.

Katika ilani hiyo, serikali ya Kenya haikutoa sababu zozote za hatua hiyo.

Marufuku hiyo inajiri siku chache baada ya Qatar kufanikiwa kurejesha uhusiano wa kidiplomasia katika ya Mogadishu na Nairobi.

Somalia ilirekebisha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya baada ya miezi mitano kufuatia upatanishi na Qatar chini ya uongozi wa Emir Sheikh Tamim Al Thani.

Wizara ya Habari ya Somalia ilisema walikuwa wakianza tena uhusiano "kwa kuzingatia masilahi ya ujirani mwema".

"Serikali mbili zinakubali kuweka uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizi mbili kwa msingi wa kanuni za kuheshimiana kwa enzi kuu na uadilifu wa eneo, kutokuingiliana katika maswala ya ndani ya kila mmoja, usawa, faida ya pande zote na kuishi kwa amani," ilisema taarifa hiyo.

Kukiri maendeleo hayo, wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Kenya ilisema inatazamia kuendeleza uhusiano wa kawaida na mamlaka ya Somalia.