Bintiye naibu rais, June Ruto aasi ukapera

Muhtasari

• June ambaye ni afisa mkuu wa ubalozi wa Kenya nchini Poland, siku ya Jumamosi alifanyiwa hafla ya posa kuambatana na mila za Jamii ya Kalenjin ijulikanayo kama ‘Koito’.

• June alimtambulisha mchumba wake Hamad Bin Khalifa aliyeandamana na familia yake katika hafla ya kufana na ambayo pia ilihudhuriwa na wandani wa naibu rais.

Bintiye naibu rais William Ruto, June Ruto ameamua ameasi maisha ya upweke na kuamua kwenda zake nchini Nigeria, baada ya kumpata mchumba kutoka Nigeria.

June ambaye ni afisa mkuu wa ubalozi wa Kenya nchini Poland, siku ya Jumamosi alifanyiwa hafla ya posa kuambatana na mila za Jamii ya Kalenjin ijulikanayo kama ‘Koito’.

June alimtambulisha mchumba wake Hamad Bin Khalifa aliyeandamana na familia yake katika hafla ya kufana na ambayo pia ilihudhuriwa na wandani wa naibu rais.

Hafla hiyo ilihusisha majadiliano kuhusu kiwango cha mahari ambacho kinafaa kutolewa kuambatana na tamaduni za jamii ya Kalenjin.

Meza ya habari ya Radio Jambo inamtakia June Ruto ndoa yenye fanaka na yenye baraka zake Mwenyezi Mungu.