Tahadhari! mvua kuendelea wiki hii Nairobi na sehemu zingine za nchi

Muhtasari

• Jumanne na Jumatano, kaunti itapata mvua nyepesi na mvua za wastani siku nzima na joto la juu la nyuzi joto 25.

• Nchi imekuwa ikishuhudia mafuriko katika maeneo mengi huku mvua ikiendelea kusababisha maafa.

Image: MAKTABA/KENHA

Wakazi wa Nairobi watakuwa na wiki iliyojaa mvua kulingana na utabiri wa siku tano wa Idara ya Hali ya Hewa.

Kaunti ya Nairobi itapokea mvua za wastani leo kutoka saa kumi na mbili asubuhi hadi sita mchana na mvua za wastani kutoka alasiri hadi saa kumi na mbili jioni.

Katika utabiri wake, Idara ya utabiri wa hali ya hewa ilisema Nairobi itapata joto la juu la nyuzi joto 24 na kiwango cha chini cha nyuzi joto 17.

Jumanne na Jumatano, kaunti itapata mvua nyepesi na mvua za wastani siku nzima na joto la juu la nyuzi joto 25.

Siku ya Alhamisi, mvua za wastani pamoja na mvua nyepesi zitashudiwa huku mvua nyepesi ikinyesha siku ya Ijumaa.

Vipindi vya jua vitashuhudiwa Ijumaa saa sita mchana.

Nchi imekuwa ikishuhudia mafuriko katika maeneo mengi huku mvua ikiendelea kusababisha maafa.

Huu ni mwanzo wa mvua ndefu za Machi-Mei ambazo zilianza wiki ya pili hadi ya tatu ya Machi.

Mvua kubwa inatarajiwa kuendelea kunyesha sehemu nyingi za nchi. Idara ya utabiri wa hali ya hewa ilisema Wakenya wanapaswa kuchukuwa tahadhari kuhusu visa vya mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Wiki iliyopita, nyumba na mashamba viliharibiwa na maporomoko ya ardhi katika eneo la Wanjerere kaunti ya Murang’a.