DRAMA KABUCHAI

Mbunge Barasa avamiwa mazishini Bungoma

Mbunge huyo alikuwa anamkashifu Gavana Wangamati alipovamiwa jukwaani na msaidizi wa Gavana na kupokonywa kipaza sauti.

Muhtasari

•Barasa aliwaambia waombolezaji kuwa walifanya makosa kumchagua Wangamati

•Sio mara ya kwanza Barasa anahusika kwenye vita hadharani

Mbunge wa Kimilili Didimus Barasa
Mbunge wa Kimilili Didimus Barasa

Kizaazaa kiliibuka siku ya Jumamosi  kwenye mazishi yaliyofanyika eneo bunge la Kabuchai, kaunti ya Bungoma baada ya mwombolezaji mmoja anayedaiwa kuwa  mmoja wa wasaidizi wa Gavana Wycliffe Wangamati wa Bungoma kumvamia na kumpokonya kipaza sauti mbunge wa Kimilili, Didmus Barasa.

Mwombolezaji huyo alimvamia  Barasa kwenye jukwaa  alipokuwa anamkashifu Gavana Wangamati mbele ya waombolezaji  kwenye mazishi ya msomi alitambulika kwa jina la kitani ‘Omukhana wa University(Msichana wa chuo kikuu).

Tukio hilo liliibuka baada ya Barasa kudai kuwa wakaazi wa Bungoma walifanya makosa kumchagua Wangamati kama Gavana wao.

“Ni makosa kubwa sana tulifanya kumchagua Gavana Wangamati. Nimemuona MCA Murunga akisema kuwa serikali ya kaunti imejenga kituo cha masomo upande wa Kitai. Kituo hicho  kilijengwa na Waholanzi. Sitakubali kamwe wananchi kudanganywa!” Mbunge Barasa aliwaambia waombolezaji kabla ya nkupokonywa kipaza sauti.

Maneno hayo yaliibua hasira kwa msaidizi mmoja wa Gavana Wangamati ambaye kwa video inayozambaa mtandandaoni anasikika kumwambia Barasa, “Wewe ndio mukora” huku akimvamia na kumpokonya  kipaza sauti.

Sio mara ya kwanza mbunge huyo anapojipata kwenye vita hadharani kwani mwaka uliopita alipigwa na kikundi kilichokuwa kimechochewa na mbunge wa Dagoretti ya kusini kwenye  uchaguzi mdogo eneo bunge la Kibra.

Baadae siku hiyo mbunge huyo aliweka video kwenye ukurusa wake wa Facebook ikionyesha waombolezaji wenye hasira waki taka kumvamia msaidizi huyo wa gavana wengine wakisika wakisema akamatwe.

“Waombolezaji walikuwa wanamezea mate damu yake. Nilimpiga na kumtoa kwenye ibada ile. Kwa sasa anauguza majeraha katika hospitali ya Kimilili” Barasa aliandika.

Didmus Barasa kwenye uchaguzi mdogo Kibra
Didmus Barasa kwenye uchaguzi mdogo Kibra
Image: Hisani