Covid-19:Asilimia ya maambukizi nchini imefika 7.4% baada ya watu 431 kupatikana na corona

Muhtasari
  • Maambukizi hayo mapya yalitoka kwa sampuli 5,846 zilizopimwa saa 24 zilizopita
  • Pia watu 31  wamepona corona huku idadi jumla ya walipona ikifika 115,844

Idadi ya visa vya maambukizi ya corona nchini imefika 169,356, baada ya watu wengine 431 zaidi kupatikana na virusi hivyo.

Maambukizi hayo mapya yalitoka kwa sampuli 5,846 zilizopimwa saa 24 zilizopita.

Kesi hizo mpya zinajumuisha Wakenya 410 na raia wa wageni 21  mgonjwa wa umri wa miezi 4 na mwenye umri wa juu ana miaka 90.

Wizara ya afya imethibitisha kuwa vifo 10 zaidi vilirekodiwa huku idadi ya walioaga dunia kutokana na corona ikifika 3,097.

Pia watu 31  wamepona corona huku idadi jumla ya walipona ikifika 115,844,

Wagonjwa 1,103 kwa sasa wamelazwa katika vituo anuwai vya afya wakati 4,713 wamo katika mpango wa huduma ya nyumbani.

Wagonjwa 113 wamo katika ICU, 24 kati yao walikuwa kwenye msaada wa upumuaji, 65 kwenye oksijeni ya ziada na wengine 24 wakichunguzwa Wagonjwa wengine 98 walikuwa kando na oksijeni ya ziada kati yao 91 walikuwa katika wadi za jumla na 7 katika kitengo cha utegemezi.