Covid-19: Watu 284 wapatikana na corona,124 wapona,17 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imerekodi visa 284 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,540 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 171, 942
Waziri wa afya Mutahi Kagwe

Kenya imerekodi visa 284 vipya vya maambukizi ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 4,540 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 171, 942.

Katika visa hivi vipya, 272  ni raia wa Kenya huku 12  wakiwa raia wa kigeni, 229 ni wa kiume na 203 ni wanawake.

Vile vile watu 124 wamepona virusi vya corona,27 walipona wakiwa nyumbani huku 97 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 117,469 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 17 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,240 watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,207 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,946 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 97 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).